M-PESA imeanza kupoteza mwelekeo na kukosa uaminifu. Nimehamisha fedha kutoka akaunti yangu ya M-PESA kwenda Akaunti ya Benki. Kilichotokea ni kuwa fedha imekatwa M-PESA lakini haijafika kwenye akaunti yangu. Pamoja na kufanya ufuatiliaji naona nazungushwa tu. Wadau naombeni ushauri nifanyeje. Nimewasiliana na Benki yangu wamenieleza kuwa wao hawashughuliki na fedha ambazo hazijaingia katika system yao. Chonde chonde Voda nirudishieni fedha zangu siwezi kuvumilia kuona fedha yangu yote ile ipotee hivi hivi wakati nimevuja jasho la haki kuipata. NB: Sikukosea kuandika akaunti namba yangu, sasa iweje fedha isiingie kwa zaidi ya masaa 72??????