GE2025 Nimepoteza interest na uchaguzi wa 2025 baada ya baadhi wagombea wa upinzani kuhamia CCM

GE2025 Nimepoteza interest na uchaguzi wa 2025 baada ya baadhi wagombea wa upinzani kuhamia CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Uchaguzi wa mwaka huu umeibua mambo ya kushangaza. Licha ya kutokuwepo kwa uwanja sawa wa ushindani wa kisiasa kati ya CCM na vyama vya upinzani, kumetokea hali ya baadhi ya wagombea waliopitishwa na vyama vya upinzani katika ngazi za udiwani na ubunge wakiwemo wale waliokuwa na ushawishi mkubwa majimboni kujiunga na chama tawala (CCM). Wamekuwa wakitoa sababu mbalimbali kama kutafuta ukurasa mpya wa siasa, kukubaliana na sera za CCM, au kumuunga mkono mgombea wa CCM.

Soma > Mgombea Ubunge ACT-Wazalendo, Hamad Hashimu, ahamia CCM

Kitendo hiki kimeibua hisia za usaliti, kwani kinadhoofisha harakati za mageuzi na kwa kiasi fulani kudharau wananchi waliowapa dhamana kupitia mchakato wa vyama vyao. Ni jambo linaloibua maswali makubwa: inawezekanaje chama kitumie muda na rasilimali kumteua mgombea, kisha ghafla huyo huyo abadili msimamo wake na kujiunga na chama tawala? Hali hii inawafanya wananchi kujiuliza kama wagombea hawa wanauzwa au wamenunuliwa kisiasa.

Pia soma > Mgombea Udiwani CHAUMMA Kata ya Liganga atimkia CCM

Mabadiliko haya yanaweka mazingira mapya kuelekea uchaguzi mkuu. Kwa upande mmoja, ushindani unaweza kupungua katika baadhi ya majimbo; kwa upande mwingine, hali hii inafunua udhaifu katika uimara wa vyama vya upinzani, msimamo wa wagombea, na kwa upana zaidi mustakabali wa siasa shirikishi nchini.

Soma > Salma Kikwete arahisishiwa Kazi Jimboni, Mgombea Ubunge CHAUMMA, Mchinga, Yusuph Tamba atimkia CCM
 
Kati ya chaguzi ambazo zimepoa kupita kawaida ni huu. Na ndio uchaguzi pia wenye badget kubwa kabisa ya pesa kuliko zote. Yaani lugha gongana kabisa
 
Back
Top Bottom