Nimepoteza kadi mbili ndani ya daladala za Mbezi/Makabe

Nimepoteza kadi mbili ndani ya daladala za Mbezi/Makabe

Hajto

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2013
Posts
5,646
Reaction score
5,606
Habari zenu mabibi na mabwana, juzi Jumapili nikiwa maeneo ya Mbezi nikielekea Makabe nikadondosha kadi zangu mbili ya bank na leseni ya udereva.

Msaada ninaoomba kwa mtu anayemjua dereva ama konda kwa ruti ya Mbezi/Makabe anipatie niwasiliane nae aniangalizie huenda wakawa wameziona hizo kadi na kwangu itakuwa msaada sana.

Tafadhalini jamani, naombeni msaada wenu.
 
Hapa hakuna Jinsi inabidi ujitaje tu majina halisi ili upate urahisi wa kuzipata
 
Kwanini usiende kwenye hivyo vituo ulivyopandia Daladala na kushukia ili uonane nao wewe mwenyewe hao Makonda/Madereva? Hiyo ndio njia rahisi zaidi kwa kuanzia,au nenda kituo chochote cha Polisi eneo hilo huenda Kadi zako zilisalimishwa huko.
 
Aisee vijana siku hizi hopeless badala ya kurudi Happ fasta umekalia kuandika JF as if wote tunaishi Makabe
 
Shukrani sana kwa ushauri wako
 
Aisee vijana siku hizi hopeless badala ya kurudi Happ fasta umekalia kuandika JF as if wote tunaishi Makabe
Nimeanzia hapa kwanza,weeknd nategemea kwenda tena hapo mbezi
 
Mkipanda daladala hakikisheni mnachukua tiketi. Mm hata kama nashuka kituo cha karibu huwa nadai tiketi ingawa abiria wengine huniona mkorofi. Pole kwa yaliyokupata
 
Mkipanda daladala hakikisheni mnachukua tiketi. Mm hata kama nashuka kituo cha karibu huwa nadai tiketi ingawa abiria wengine huniona mkorofi. Pole kwa yaliyokupata
Daladala za kule hazitoi tiketi,
 
Mkipanda daladala hakikisheni mnapewa tiketi. Mimi nikipanda daladala hata kama nashuka kituo cha karibu huwa nadai tiketi ingawa abiria wengine huniona mkorofi. Jambo lolote laweza kutokea safarini, mfano AJALI. Panapotokea ajali raia huenda eneo la tukio. Kama hujachukua tiketi utajulikanaje kama wewe no miongoni mwa wasafiri. Unaweza kukosa haki zako kama vile kulipwa BIMA n. k
 
Back
Top Bottom