Nimepoteza kadi ya Benki, baada ya muda nikaanza kupokea SMS za miamala kwenye simu yangu. Hili jambo linawezekanaje?

Nimepoteza kadi ya Benki, baada ya muda nikaanza kupokea SMS za miamala kwenye simu yangu. Hili jambo linawezekanaje?

Lower key

Member
Joined
Mar 24, 2025
Posts
18
Reaction score
14
Wakuu, habari za muda huu.

Naleta mada hii mbele yenu nikiwa na taharuki, lakini lengo langu ni kupata uelewa na maarifa kutoka kwenu wataalamu.

Siku chache zilizopita nilipoteza kadi yangu ya ATM (kadi ya benki). Wakati bado nahangaika kufikiria jinsi ya kwenda benki kuifungia (block), ndani ya muda mfupi nilishangaa kuanza kupokea jumbe fupi (SMS) kwenye simu yangu zikionyesha kuwa kuna kiasi fulani cha pesa kinatolewa na kuhamishwa kutoka kwenye akaunti yangu.

Kitu kinachoniumiza kichwa na kuniweka katika sintofahamu ni hiki:
  1. Kadi yangu haikuwa na PIN namba yoyote iliyoandikwa juu yake, na sikuwa nimeandika sehemu yoyote ambayo mwizi angeweza kuipata.
  2. Miamala ile haikuwa inafanyika kwenye mashine ya ATM (ambapo ungehitaji kadi na PIN), bali meseji zilikuwa zinaonyesha muamala umerushwa kwa njia ya Mobile Banking au USSD.
  3. Simu yangu ninayo mkononi, haijapotea, ina mtandao na haijaguswa na mtu yeyote.
Maswali yangu makubwa kwenu wajuzi wa mambo:
  • Mwizi anawezaje kutumia kadi ya benki pekee kuanza kufanya miamala inayofika hadi kwenye simu yangu wakati simu ninayo mkononi?
  • Je, kuna teknolojia gani au mbinu gani ya kiuhalifu inayoweza kuunganisha data za kadi ya ATM na Mobile banking bila mimi mwenyewe kuhusika?
Naomba nondo zenu na msaada wenu wakuu, ili mimi na wengine wanaoweza kukumbana na hili tujue jinsi ya kujilinda na jinsi mifumo yetu inavyofanya kazi.
 
Hiyo Kadi Kuna MTU anaejua No. yako ya siri amekupiga au

Tho Kuna app moja ya kubook hotels n.k inakubali malipo ya card yoyote hata bila address ya mwenye kikubwa iwe na cvv tu

sometime pia huenda wafanyakazi wa benk husika wameamua kutake advantage sababu si wote ni waaminifu.

Nenda bank husika
 
Wezi wa simu na porch kuna namna wapo connected na mawakala wa pesa mitaani na hawa mawakala wana watu wao inside kwenye mitandao hii tunayoiamini so mitandao ya simu sijui bank siyo wa kuwaamini hata kidogo.

April 29th mwaka huu majira 19:25 niliibiwa simu pale Fire Dar yenye line mbili Vodacom na Airtel simu ilichukuliwa katikati ya lundo la watu kwa wanaojua usafiri wa Dar nyakati za jioni wanaelewa,nilikuwa napanda bus (Mwendokasi) so nikaja kugundua nimeibiwa nikiwa Manzese haraka sana nikaomba abiria mwenye Voda anisaidie nipige huduma kwa wateja nia waifunge line yangu ila kwa sababu ya usumbufu namna ya kuipata line nizungumze na muhudumu Voda wamejaza mi-bot tu kila namba nayobonyeza siwapati nilipofika Kimara mbio mbio nikaenda kwa wakala ku-renew line zangu muda huo ni 19:51 nilipofika home Mbezi nikaziweka line kwenye simu ya ziada ili maisha mengine yaendelee but nikapokea sms kutoka M-pesa kwamba "Nimesongesha/Kopa" Tsh 320,000/=.

So nikachukua jukumu la kukomaa sasa kuwatafuta Voda kwa namba yangu lengo kujua nimekopa saa ngapi (nilishahisi kuna namna mwizi amecheza na line zangu) kuwapata wananiambia nilikuwa maeneo ya Gerezani saa 19:37 nikaenda kwa wakala kutoa hela Tsh 650,000/= salio halikutosha nikasongesha hiyo 320K nikatoa pesa 650K saa 19:45 so wakati mimi nipo Ubungo nahangaika kuwatafuta kuomba msaada wafunge line yangu mwizi kupitia wakala Gerezani walikuwa wanawasiliana na watu wao ndani ya Vodacom kupata taarifa za line yangu PUK Pin na M-pesa password,(Kumbuka simu ina password so jaribio lolote la kutumia line yangu lingefanyika nje ya simu yangu so kitendo cha kuweka line kwenye simu nyengine line ingedai PUK)

Nasema hivi kwa sababu baada ya malumbano makali sana na yule mwanamke customer service wa Voda mimi nikiukana huo muamala huku yeye akisema ni mimi nimeufanya nikamuuliza je,nilipokuwa natoa pesa hata ikaonekana salio halitoshi nikakopa then nikatoa tena nikafanikiwa niliingiza namba ya siri mara ngapi (lengo langu kujua huyu mwizi alijaribu mara ngapi kubuni password) akaniambia miamala yote niliifanya kwa usahihi sikukosea namba ya siri hata mara moja moja kwa moja nikajua kuna uhuni umefanyika na nina jamaa zangu watatu niliwashirikisha wote wamewahi kukutana na same problem.

Washenzi sana hawa watu!
 
Wewe sema unataka kufundishwa namna ya kuwaibia watu kwa ATM card zile za tuma kwenye namba hii saivi watu hawashtuki nazo.
 
Eleza vizuri hapa imekuwaje siri sio siri
Alichoandika Sisyphus ni kitu clearly kabisa yaani kipo wazi nashangaa post yake ni kama mods wamei-hide ila ni ukweli kinachoitwa namba za siri hakipo.

Unayoamini ni namba yako ya siri ni watu tu hawajapata chance ya kuitumia siku wakiwa na kazi nayo kilio utakitoa kama mtoto mchanga take it from me.
 
Wezi wa simu na porch kuna namna wapo connected na mawakala wa pesa mitaani na hawa mawakala wana watu wao inside kwenye mitandao hii tunayoiamini so mitandao ya simu sijui bank siyo wa kuwaamini hata kidogo.


Washenzi sana hawa watu!
Huu ufanyike kuwa uzi mkuu watu wajue wawe makini zaid
 
Wakuu, habari za muda huu.
Naleta mada hii mbele yenu nikiwa na taharuki, lakini lengo langu ni kupata uelewa na maarifa kutoka kwenu wataalamu.

wakuu, ili mimi na wengine wanaoweza kukumbana na hili tujue jinsi ya kujilinda na jinsi mifumo yetu inavyofanya kazi.
Kama maelezo yako ni sahihi, kuna uwezekano mkubwa kuwa tatizo halikusababishwa na kupotea kwa kadi peke yake. Kupotea kwa kadi na kuanza kwa miamala huenda ni matukio yaliyotokea kwa wakati mmoja lakini chanzo kikawa tofauti.


Baadhi ya uwezekano ni:


  • Akaunti ya Mobile Banking au USSD ilishawahi kuingiliwa kwa njia ya ulaghai, mfano mtu kupata taarifa zako kwa njia ya phishing au kujifanya afisa wa benki.
  • Kulikuwa na ubadilishaji wa SIM (SIM swap), ambapo namba yako ilihamishiwa kwenye SIM nyingine kwa muda na kutumika kufanya miamala.
  • Mtu alikuwa tayari anafahamu taarifa muhimu za akaunti yako kabla hata hujapoteza kadi.
Kwa kawaida, kadi ya ATM pekee haitoshi kumwezesha mtu kuingia kwenye Mobile Banking au USSD na kufanya miamala. Mifumo hiyo mara nyingi huhitaji usajili, uthibitisho wa namba ya simu, PIN ya huduma au hatua nyingine za usalama.

Cha muhimu kufanya mara moja ni:
  1. Wasiliana na benki na uombe wafungie kadi pamoja na huduma za Mobile Banking.
  2. Omba historia (logs) za miamala ili kujua ilifanyika kupitia njia gani hasa.
  3. Badili PIN zote za benki na Mobile Banking.
  4. Wasiliana pia na kampuni ya simu ili kuthibitisha kama hakukuwa na tukio la SIM swap.

Ukipata taarifa kutoka benki kwamba miamala ilifanyika kupitia Mobile Banking ilhali hukuwa umeidhinisha, ni muhimu benki ifanye uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha tatizo.
 
Umepoteza card na hujatoa taarifa kwa bank yako waifunge account kwa muda, sawa basi subiri hadi hela zote ziishe kwenye account
 
Back
Top Bottom