Ushauri wangu ni huu,kama unafamilia hakikisha unanunua chakula kwanza mfano,mchele,sembe,mafuta,sukari,mkaa,gas n.k,Ili usije kuanza kuhangaika hata kukosa chakula Kwa kipindi hiki Cha mpito na kujitafuta upya,Tenga LAKI 2 na NUSU Hadi 300k jifunze udereva wa Bajaj,hiyo pesa utaitumia kupata leseni na connection ya chombo Cha kuendesha.Niamini Mimi ukishajua kuendesha Bajaj hutalala njaa wala hutakuwa na stress za pesa ya matumizi.Sijui mkuranga ni mji wenye mishemishe kiasi Gani lakini ukisogea mji uliochangamka karibu na hapo kwako hii mbinu itakusaidia kukabiliana na hustling za kila siku.Jitahidi hiyo pesa usiivuruge kabla hujafanya kitu,itumie kama daraja la angalau kukupa matumaini ya siku za usoni wakati unasubiri fursa zaidi.