Nimerejea kutazama 'Video' mbalimbali za Hayati Rais Dkt. Magufuli niseme tu Samahani kwa 'Kumkosoa' ila Asante Mungu kwa 'Kutuzawadia' Rais kama yeye

Mtu ametawala miaka mitano tu lkn tuliona nchi ikibadilika ki maendeleo hasa kwenye miundo mbinu........
CDM walivyokuwa wanafiki eti wanakwambia tunataka maendeleo ya watu sio vitu.......maendeleo ya watu utapataje bila maendeleo ya vitu!!??
 
Kweli siamini kama niwewe uliyeandika hapa


Ila HONGERA KWA KUTAMBUA UKWELI
 
Nchi zilizoendelea ukiondoka madarakani au ukifariki wanakuwa wamemaliziana na wewe, sisi tunaendelea kuwa na matumaini kuwa atatukomboa!
Heshimu Mtizamo wangu na Mawazo yangu. Sasa kama unajua kuna nchi nyingi tu zilizoendelea na Unazipenda huenda unatamani hata Raia wao kwanini usiende Kuishi nao huko na ukatuachia tuendelee Kuipambania Tanzania yetu na Kuwalilia akina Nyerere, Mkapa na Dkt. Magufuli?
 
Itachukua miaka mingi kumpata kama JPM.
Nakubaliana nawe tena 200% kabisa Mkuu. Nimechukua muda Kurejea 'Video' zake na Kugundua ya kwamba Mwenyezi Mungu alitupa Zawadi ya Thamani Hayati Rais Dkt. Magufuli na akaichukua mapema baada ya Kutuona Watanzania hatujamshukuru na Kuishukuru pia.

Hata Machozi yalinitoka sana tu Mkuu.
 
Post yako tu hii imenifanya nianze Kulia.
 
Amen!!Amen!!Amen!!
 
Mkuu popote pale ulipo kwa post yako hii naomba nikupigie 'Salute' ya Heshima tena ile ya Kijeshi kabisa.

Hii post yako ingekuwa ni bidhaa inayouzwa hata kama ingekuwa ni Milioni ningejitajidi Kuinunua.

Umeandika vyema na Ukweli mtupu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…