Nimerudi kwa mke wangu

Nimerudi kwa mke wangu

Mkulungwa01

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
3,977
Reaction score
5,339
Miaka 4 iliopita nilikuwa mlevi wa kupindukia, nilimtesa sana wife, kurudi saa 9 usiku kwa sana, umalaya n.k, hom nilikua naacha 2000 na tuna watoto 3, wife alilalamika snaa na mwisho nikahama hom bila hata kuwaachia chochote. Ni miaka 3 imepita.

Apa naomba nikiri kua nilikula sana raha, bahati mbaya nikafilisika na sasa nimerudi kwa wife. Nimejifunza na sitorudia, asante wife kwa kunipokea na kunizalia mtoto mwingine. Wewe ni mama lamama yaani loooh, now ni mwendo wa nyama samaki tu, jaman kuoa mke mwenye akili rahaamno, ila najuta kwa nilichofanya
 
Wew ndo baharia sasa salute kwako...

Na uzee wako utakua mzuri mnoo endapo hautoludoa hayaa!!!!

Salute kwa mkeo!!!

I hope utainuka tena mpyaa ulopitia mabaya!!!
 
Miaka 4 iliopita nilikuwa mlevi wa kupindukia, nilimtesa sana wife, kurudi saa 9 usiku kwa sana, umalaya n.k, hom nilikua naacha 2000 na tuna watoto 3, wife alilalamika snaa na mwisho nikahama hom bila hata kuwaachia chochote. Ni miaka 3 imepita.

Apa naomba nikiri kua nilikula sana raha, bahati mbaya nikafilisika na sasa nimerudi kwa wife. Nimejifunza na sitorudia, asante wife kwa kunipokea na kunizalia mtoto mwingine. Wewe ni mama lamama yaani loooh, now ni mwendo wa nyama samaki tu, jaman kuoa mke mwenye akili rahaamno, ila najuta kwa nilichofanya

Wanawake Mungu alijua kutuumba na mioyo ya kusamehe

Ila usirudie tenda kumtesa maana wengi wetu siku tukichokaga ndio yale mambo ya kupita na ⛽🔥 na kuishia kugawana majengo ya serikali

Ishi nae kwa akili
 
Mwanaume unayeikimbia familia yako utakua wa hovyo sana wewe, hili nakuambia kama mwanaume mwenzio, huwa tunayafanya mengi lakini tunalinda sana familia zetu, tunawapa matunzo na kujaribu kila jitihada za kuhakikisha hatuleti ukimwi nyumbani.
Haya maisha, ipo siku utazeeka na kuwa mnyonge, familia yako ndio itakua nguzo lako, hivyo leo unazo nguvu na uwezo wa kupanda utakachovuna miaka ya baadaye.
 
Inawezekana umekuwa kama likobe lililoficha kichwa kwenye gamba kwa kuwa huna miamala natabiri miamala ikianza kusoma utatoa kichwa nje kwa mwendo uleule wa likobe
 
Back
Top Bottom