Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Dude, leo umeamkia upande upi? Mpaka sasa umeshakamata tuzo kadhaa za wema na utu toka kwangu!
mazee kwani unaijua ratiba ya regia? Kwani regia ndo alienda kilombero wakati wa uchaguzi tu na huko siku za nyuma na miaka ya nyuma alikuwa hajawahi kwenda? Au kakwambia ndo keshaondoka for good?
bila ya shaka natia shaka ndo maana nikauliza suali. Natia shaka ya kwanini chadema ikaruhusu hali hiyo itokee.
msikiko wa sauti ni kwa mujibu wa akili yako ulivyoiweka, Asprin kasikia uzuri na akatoa jibu muafaka mbona.
mi naamini hoja ya msingi hapa ni KUMKARIBISHA,mheshimiwa regia jamvini......!
mambo mengine naona huyo kiranga anakuwa too theoretical!
for your information kiranga ni kwamba regia ATAINGIA BUNGENI!
karibu sana dada-lake-na-mimi!
achana na ''siasa-za-vitabuni'' za huyo kiranga!
TUNAANDAA KIKAO KIKUBWA SANA NA POMBE NYINGI SANA katikati ya wiki....!hiyo ndo kazi yangu bwana
Kwanza unajua primary domicile yake ni wapi?
ha ha ha!Hoja ya msingi ni kwamba kulazimisha hoja fulani ni hoja ya msingi si hoja ya msingi.
Labda kama uko tingas tayari.
Kiranga bana, kumbe una bifu za watoto wa sekondari. Just one question do u think Regia would be interested in your type of criticism on her?
If you have some genuine concerns as to how she should be running her life after elections why don't you contact her privately? After all who r u to determine how close and the manner of closeness a candidate should be with the electorate?
Huyu dada anastahili pongezi kwanza kabla hata ya kuanza kumcriticize, wht she has done probably most of us will never do it in our lives! Ameingia kwenye vitabu vya historia na still she's a potential of becoming a Kilombero MP in some near future. Ameweza kuthubutu kufanya kile ambacho most of theople including you Kiranga thought it was impossible. Wengi wenu humu mtaishia kuandika mivolyumu na mivolyume ya makaratasi ambayo yatabaki humo humo kwenye makaratasi,
Mtu hata hajapumzika tayari ng'e ng'e mmh! mha he! ng'iii.................kwa kifupi sio ustaarabu.
mimi sijui. Wewe unajua?
mimi sipendi manyanyaso na uonevu aisee. Dada wa watu kapigana kufa na kupona huko kilombero licha ya mizengwe aliyokumbana nayo halafu anarudi hapa kutujulia hali halafu anaanza kushambuliwa bila sababu ya msingi. Lazima nimkingie kifua. Dada wa watu hajatamka ana mipango gani lakini tayari watu washaanza kumpangia. Ila diana wa pale calabash kachangia sana huu wema (teamo anamjua huyu). Wako katika ujenzi wa taifa nn aka mzee wa byuroo lol
Hii concept nzima ya "kurudi" kutoka Kilombero mimi napata tabu nayo sana. Inaonekana Kilombero -pamoja na majimbo mengine ya vijijini- ni sehemu za kwenda wakati wa uchaguzi tu, uchaguzi ukiisha watu wanarudi kwenye shughuli zao za kawaida mijini.
Badala ya wagombea walioshindwa mwaka huu kubaki huko vijijini kuimarisha vyama vya upinzani, kuisadidia jamii pamoja na kupanga mikakati ya kushinda hivi viti katika uchaguzi ujao, tunaona increasingly "wanarudi" mijini.
Wapinzani wakiendelea kushindwa katika kila chaguzi zijazo watashangaa kweli kwa mwendo huu wa kwenda majimboni nyakati za chaguzi tu, na chaguzi zikiisha wanarudi mijini kwenye mitandao na urahisi wa maisha ?
Tunawatendea haki wananchi kweli kwa mwenendo huu ?
haswaa na wala hujakosea. Nasikia na kuelewa kwa mujibu wa masikio na akili yangu na aspirin na wengineo nao vivyo hivyo.
mimi sijui. Wewe unajua?
Kama hujui huna haki ya kubishia hoja zangu kuhusu wawakilishi na wadau wanaojinadi kutaka uwakilishi kuwa karibu na wananchi, mimi najua Regia Kilombero si primary domicile yake.
speed in a wrong direction is irrelevantTofauti kati ya Kiranga na Regia Mtema ni kwamba, Kiranga hajawahi kugombea nafasi ya kutaka kuwawakilisha wananchi wa Kilombero, kwa hiyo hana haja wala wajibu wa kuwa karibu na watu wa Kilombero.
Lakini Regia Mtema ndiyo kwanza anatoka kugombea ubunge na ameonyesha kuwa mdau mkubwa wa watu wa Kilombero.
Wanaotaka dhamana kubwa kutoka kwa wananchi inabidi watuonyeshe kwamba wanafanya kazi kubwa na wananchi hawa, vile vile wasiotaka dhamana hata ndogo kutoka kwa wananchi hawa, watu kama kina Kiranga ambao hawana ndoto ya kugombea public office, hawana wajibu wa kuwa karibu na wananchi hawa. Wakifanya hivyo kwa matakwa yao ni sawa, lakini pia wana haki na uhalali wote wa kuingia katika spaceship na kwenda Andromeda Galaxy for all that we care.
You can't eat your cake and have it still. Huwezi kujinadi kama mdau mkubwa wa watu wa Kilombero, halafu uchaguzi ukiisha wiki moja tu unajitoa Kilombero na "kurudi" mjini kwenye uafadhali wa maisha. Kama unaishi kwenye uafadhali huu wa maisha utapata wapi uchungu wa kudai uafadhali huu wa maisha wa mjini ufike vijijini?
Ndiyo maana vijijini hakuendelei, wabunge wote na wapinzani wao wako mijini, wanaenda vijijini nyakati za chaguzi tu.
please share with us your experience huko ulaya na marekani wanaoshindwa wanafanyaje na pia uelewa wako wa siasa za bongo kama ni full time hata pale unapokosa nafasi
a uniderectional mind is a confined one
ujuaji ukizidi....
ukijua hilo, mambo ya kujifunza yametokea wapi?

Kupumzika baada ya kampeni ni lazima kuondoka Kilombero ? Kama mtu una haja ya ku represent kweli watu wa Kilombero unapumzika wanavyopumzika wao huko, unawajua vizuri.

Sio mtu unataka kuwawakilisha watu wa Kilombero mapumziko yako dunia tofauti na yao. Huu si umamluki ninaousema hapa?

Ukisema Regia kaamua kuja mjini kwa sababu kaamua siasa tena yeye basi utakuwa unakubali kwamba Regia alikuwa hana interest ya moyoni kusaidia maendeleo Kilombero, alikuwa anatafuta ajira tu na ukubwa sasa imeshindikana hana muda wa kupoteza huko bush.

Mtu mwenye nia ya kuleta maendeleo Kilombero hata akishindwa ubunge atatafuta namna nyingine ya kufanya kazi na watu wa huko, sio kuwakimbia wiki moja baada ya uchaguzi.
.......ukweli kwamba wapinzani wetu hawakujiandaa vilivyo na waliweka wagombea dhaifu kama kina Regia. ......