A
Anonymous
Guest
Mi ni mmoja wa wananchi tuliotekeleza maelekezo ya National Identification Authority (NIDA) ya kurudisha vitambulisho vya Taifa vilivyokuwa na tatizo la kufutika kwa majina au namba ili vibadilishwe na kutolewa vingine visivyo na changamoto hiyo.
Nilirudisha kitambulisho changu tangu mwezi Januari katika Ofisi za NIDA Mkoa wa Morogoro, zilizopo Kata ya Tungi, Morogoro Mjini. Hata hivyo, hadi sasa sijapokea kitambulisho kipya, wala hatujapewa taarifa rasmi kuhusu lini vitambulisho hivyo vitakuwa tayari.
Kila tunapokwenda ofisini kufuatilia, hatupati majibu ya kueleweka. Pia, tangu zoezi la kurejesha vitambulisho lilipoanza, mamlaka haijatoa taarifa nyingine kuhusu maendeleo ya uchapishaji au ugawaji wa vitambulisho vipya kwa wananchi walioathirika.
Kuchelewa huku kumetusababishia usumbufu mkubwa, kwani kwa sasa Kitambulisho cha Taifa kinahitajika katika huduma nyingi muhimu, ikiwemo safari, huduma za kifedha, ajira na shughuli nyingine za kila siku. Kukosa kitambulisho halisi kumeathiri uwezo wetu wa kupata huduma hizo kwa wakati.
Kupitia ujumbe huu, tunaomba NIDA itoe taarifa rasmi kwa wananchi kuhusu hatua iliyofikiwa katika zoezi la kubadilisha vitambulisho hivyo, pamoja na kutangaza lini waliorejesha vitambulisho vyao wataanza kuvipokea.
Tunaiomba mamlaka husika kulipa uzito suala hili ili wananchi wasiendelea kupata usumbufu katika kupata huduma muhimu zinazohitaji Kitambulisho cha Taifa.