Nimesababisha depression kwa mtoto wa watu

Nimesababisha depression kwa mtoto wa watu

hopetumaini

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2013
Posts
528
Reaction score
316
Habari za jioni wapendwa.

Mimi ni mtumishi wa afya katika moja ya hospitali zilizoko jiji la Makalla. Mwanzoni mwa wiki iliyoisha alikuja mrimbwende mmoja kumuuguza rafiki yake aliyekua kalazwa hospitalini kwetu.

Nilimwelewa sana huyu mlimbwende nikajisemeha huyu mtoto siwezi muacha hivihivi. Nilipambana mpaka nikapata namba, tukaanza wasiliana, nikamtemea mistari akajaa. Tukakubaliana weekend ya jana jpili aje kunisalimia magettoni ( kumchakata). Japo nilimgusia swala la kupima afya zetu akakubali bila ubishi.

Sasa jana mtoto katimba nikamkaribisha vizuri magettoni, story mbili tatu hivi, baadae nikamuuliza tunaweza kucheki afya zetu akakubali nikatoa vipimo na kuanza kumpima yeye kwanza. Majibu yalitoka yenye mkanganyiko, kipimo kilisoma kwenye T na C ikabidi nitulie baada ya muda nikarudia tena na majibu yakaja kama ya kwanza. Nilitumia ORAQUICK HIV SELF-TEST.

Kiukweli stimu za kumgegeda zilikata nikabaki tu nampigisha story. Japo alianza kulia pale nikambembeleza akatulia. Nikamwambia majibu si kwamba una HIV bali unahitaji kipimo cha kutumia damu. Nikamshauri akiwa tayari anaweza kwenda kituo cha afya karibu yake au akaja napofanya kazi tukamcheki zaidi.Alinyong'onyea sana mpaka nikajuta kwann nilimpima.
Aliondoka akiwa mnyonge sana.

Leo nimeongea nae kashindwa kwenda kazini mawazo yamemjaa na hukula toka asubuhi, imebidi jioni hii ninunue msosi na kumpelekea anapoishi. Kwa sasa naondoka narudi magettoni lakini sina amani, amejawa na mawazo sana japo nimemshauri vya kutosha kwamba majibu hayakuonesha kwamba ana HIV lakini imekua ngumu kwake kuelewa. Naogopa asije fanya maamuzu mabaya, mbaya zaidi anaishi mwenyewe.
NIKOSA AMANI JUU YA HUYU BINTI WA WATU.

JPEG_20210614_215716_650258521088794391.jpg
 
Habari za jioni wapendwa.
Mimi ni mtumishi wa afya katika moja ya hospitali zilizoko jiji la Makalla. Mwanzoni mwa wiki iliyoisha alikuja mrimbwende mmoja kumuuguza rafiki yake aliyekua kalazwa hospitalini kwetu.
Ungekuta non- reactive, ungesex nae. Si ndio?

Vp kama, bado antibodies hazijawa detected lakini tayari ana infection.??
 
Unafanya(ga) cyo poa mzee ... Nimewahi kuwa na jamaa yangu dk. kwa sasa marehemu. Yeye alikuwa(ga) awanapima bila kujua, akishamzimia anasubiri hadi siku akienda hospital anaumwa then anampima na STDs & HIV....
 
Hutu tukaka twenye vifaa vya kupima nyumbani ama kwenye gari tumalaya sana.

Kenge nyie.

Thread 'Mpenzi wangu anatongozwa sana!' Mpenzi wangu anatongozwa sana!

Thread 'Mchepuko wangu kaanza kuchepuka' Mchepuko wangu kaanza kuchepuka

Afu si unajifanya Dokta?

Thread 'Madhara ya dawa ya kuzuia mimba P2' Madhara ya dawa ya kuzuia mimba P2
Mkuu si kila mtumishi wa hospitali/afya ni daktari kuna wahasibu,maafisa ugavi,data officers na wengine wengi. Ndio maana sijajitambulisha kama daktari.
 
Mkuu si kila mtumishi wa hospitali ni daktari kuna wahasibu,maafisa ugavi,data officers na wengine wengi. Ndio maana sijajitambulisha kama daktari.
Na wanaofanya usafi pia ni Watumishi wa spitali.

Kila mtu acheze kivyake kwenye angle zake.

Ukute hapo umesomea Dada wa watu results ambazo sio zake ni zako 🥺🥺🥺🥺😜😜😜afu unakuja kutuhadisia
 
Back
Top Bottom