Nimeshaandaa Shamba, Nimeshapiga Mashimo ya Mahindi je, naweza kufukia mbegu kabla ya Mvua kunyesha?

Nimeshaandaa Shamba, Nimeshapiga Mashimo ya Mahindi je, naweza kufukia mbegu kabla ya Mvua kunyesha?

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,047
Reaction score
1,832
Kwa mujibu wa Mamlaka ya hali ya hewa na majira ya huku niliko, mvua za kupandia zinatarajia kuanza kunyesha wiki ya Tatu ya mwezi March ambayo ishafika mimi nimeshaandaa shamba na nimeshapiga Mashimo na nimeshanunua mbegu.

Je, naweza kufukia mbegu kabla ya mvua kunyesha?

Nahofia nisije nikafukia halafu mvua zikaja chache na mbegu zikaharibika.

Ushauri kwa wazoefu ambao wameshafanya hii kitu
 
Subiri mvua mkuu.

Kama mbegu unachota ghalani fukia Ila kama unanunua mbegu ya kisasa dukani subiri
 
Subiri mvua inyeshe Kwanza, Kisha panda. Huna haja ya kuharakisha ikiwa tayari umeshaandaa shamba.
 
Mkuu mvua ya kwanza ikishanyesha hakikisha wewe kesho yake unapanda
Baadaye kabisa utanishukuru maana wewe utakuwa wa kwanza kuvuna
 
Unaweza kufukia hiyo mbegu bila shida. Ila una uhakika na mvua itanyesha ndani ya siku 3 hadi 5 zijazo? Maana kama joto ni kali hapo chini, mbegu ikikaa ardhini muda mrefu bila kupata maji itaharibika na ni hasara kubwa hasa kama mbegu ni za dukani
 
Back
Top Bottom