Mambo mengi yamebadilika sana tokea kipindi hiko, na bepari hakutoa huo msaada bure hio ilikua ni mikopo. Hilo jambo liliwezekana kwa sababu kwa kipindi hiko duniani marekani ndo ilikua nchi yenye viwanda vingi, aliweza kuzalisha kwa wingi na akawa na soko la uhakika, hakutoa kitu bure, alikua anawekeza na mikopo alizipa nchi zote zilizokua zinapigana na mjerumani ila mrusi ndo alieweza kumdhibiti mjerumani.
Hao waingereza walishaanza kulamba pesa ya mmarekani mapema zaidi ila waliishia kulamba sakafu tu mjerumani aliwatandika akachukua hadi nchi zao kwa sasa hali ni tofauti nchi yenye viwanda vingi na inayoweza kuzalisha bidhaa kwa wingi ni china huku muhindi akimfukuzia.
Kwa hii factor ya sasa mchina na muhindi wanapata gesi na mafuta kwa bei chee zaidi kutoka kwa mrusi, mchina akigeuza kibao wamagharibi watakimbiana , na mrusi anajua karata anayoicheza ndo maana hawa jamaa kipindi hiki wamekua karibu sana, hizo silaha wamagharibi wanazopeleka ukraine lazima stock ifidiwe gharama za uzalishaji kwa nchi za magharibi zinapanda, watu wanakimbiza mwizi kimya kimya.
Itaendelea[emoji237][emoji237]
View attachment 2351907View attachment 2351908View attachment 2351909View attachment 2351910View attachment 2351911View attachment 2351912View attachment 2351913View attachment 2351914View attachment 2351917View attachment 2351918