Nimeshangaa mahindi ya kutengeneza popcorn yanatoka nje

Nimeshangaa mahindi ya kutengeneza popcorn yanatoka nje

Ya Tanzania hata hayapasuki vizuri mwisho yanaishia kuungua tu.
ninafanya biashara ya popcorn kwa sasa mahindi yamekuwa adimu na yanauzwa 6000 badala ya 4000 mahindi ya Tanzania yamejaa sokoni jana nimenunua mahindi ya bisi kwa 6000 tegeta nyuki kumbe kaniuzia ya Tanzania ambayo hayapasuki vizuri nikamrudishia ndio akanipa mahindi mazuri.
 
Mie huyanunua kwa 5000 kilo. Ya tz sio kabisaaa.
 
Kuna ndugu yangu alilima hapa Iringa, siku niliyo kuepo pale alichukua akayakaanga kweny sufuria ndogo ya kawaida na moto kidog.
Yalipasuka vzr san asilimia 98.
Mm hilo sishangai najua ndo tulivyo sisi tz tunajipang kufanya mambo makubwa tu issue ndogo tunaona upuuzi.
Mfano juzi nilienda kununua stick zile ndefu za kuchomea mishikaki, aisee nilishangaa tule tufimbo tunatoa China!!!
Nilibidi nijidharau kwanza kisha nikapiga picha hii hapa.View attachment 1478834View attachment 1478836View attachment 1478839
naomba number ya huyo jamaa wako wa iringa nataka nikayalime mbeya maana ninafanya biashara ya popcorn Dar nimeweka watu nina machine 5 sasa na huu mfumuko bei faida inakuwa changamoto
 
Tatizo kubwa linalofanya mahindi ya popcorn kutokuwa na ubora Kwa hapa nchini kweli linatokana na mambo yafuatayo
  • kuchangamana na aina nyingine za mahindi yakiwa shambani hili ni tatizo kubwa na linapelekea mbadilishano wa chavua zinazosambazwa na upepo kutoka shamba moja Hadi lingine na kuharibu ubora wa mahindi haya(cross pollination)
  • kutozingatia kiwango sahihi Cha unyevunyevu (moisture content) wakati wa kuyatunza, Ili punje ipasuke vizuri inahitaji kiwango kidogo sana Cha unyevunyevu, wenzetu wanthamini sana vitu wanavyouza nje ya nchi yao ndomaana yanapokuja huku yanakuwa na ubora wa hali ya juu, wao wanavipimo vya unyevunyevu (moisture content) .

Angalizo Kwa wanaotaka kulima
  • hakikisha shamba lako limezungukwa na mazao tofauti na mahindi pande zote nne.
  • hakikisha mahindi yako yamekauka vizuri wakati wa kuyatunza Ili kuepukana na sumu kuvu ambayo hupunguza ubora Kwa kiasi kikubwa.
  • kama eneo unalotaka kulima limezungukwa na mashamba ya mahindi, acha Yale mahindi yaote kwanza walau wiki tatu Hadi nne ndo upande mahindi ya popcorn hii itasaidia kwani kasi na hatua za ukuaji itakuwa tofauti
  • pia Kwa maeneo yenye mvua nyingi mnashauriwa kupanda mahindi haya wiki ya Tano mpaka sita ya msimu wa mvua kwani mahindi haya hayaitaji mvua nyingi, hii itayafanya yapoteze maji Kwa urahisi na kukauka yakiwa na ubora.
  • usisahau kuzingatia kanuni zingine za kilimo kama mbolea, kudhibiti wadudu, magonjwa na magugu

[emoji95] KILA LA HERI[emoji120][emoji120] Huo ni mtazamo wangu kama bwana shamba
 
wayaboi nina shamba la ekari 2 mbeya nataka nijikite kwenye kilimo cha mahindi ya bisi ila sijui pa kuanzia...yale mahindi tunayonunua dukani ndo mbegu yenyewe ukipanda yanaota?
 
wayaboi nina shamba la ekari 2 mbeya nataka nijikite kwenye kilimo cha mahindi ya bisi ila sijui pa kuanzia...yale mahindi tunayonunua dukani ndo mbegu yenyewe ukipanda yanaota?
Nenda ukanunue Yale ya sokoni, yachambue vizuri af loweka siku moja then kapande
 
wayaboi nina shamba la ekari 2 mbeya nataka nijikite kwenye kilimo cha mahindi ya bisi ila sijui pa kuanzia...yale mahindi tunayonunua dukani ndo mbegu yenyewe ukipanda yanaota?
Unafahamu sheria za kulima mahindi ya mbehu? zile mahindi Bisi zina sheria zake,sio kujilimia tu kama unalima mihogo
 
Hapa watu wanalima sana isipokuwa ubora wake unakuwa tofauti sana na yanayotoka nje.Mimi ni mtengenezaji mzuri wa popcorn ila ya ndani yanapasuka kidogo sana tofauti na yale yanayotka nje yanapasuka kwa kiwango kikubwa na kuvutia
Nahitaji kufahamu zaidi.
 
Back
Top Bottom