Nimeshangaa sana NSSF, asilimia kubwa wanaodai mafao ni vijana na si wazee kama ilivyokuwa zamani

wengi wenu huwa mnakosa supportive document ndo maana mnazungushwa kiongozi
Swala sio hilo tu, pia mnanyodo sana, unakuta mtu anakuja kudai madai yake katoka mbali mnashindwa kumsaidia unakuta kajaza vibaya fomu ambapo ni jambo la kumuomba mkae mrekebishe ila mnamwambia arudi tena akishakamilisha, unakuta ni mzee mtu kashachoka hana hata nauli, mnakosea sana.
 
Kwani mafao, bado yanatolewa, si kuna tamko Hadi mtu afikishe miaka 60.Ama Mimi nimelala usingizini bado?
Inategemea na fao gani we chalii usikariri, kuna baadhi ya mafao unachukua pesa yako kama umekidhi matakwa
 
Sio uvivu,ila mazingira na mambo kama hayo.
Uliza sasa maswali hapa usaidiwe, mazingira sio ukomo wa kupata elimu, mitandao ipo siku hizi hata ukiwa wapi unapata taarifa kamili na kwa haraka
 
Iceberg9 swali tatanishi mbona wale watumishi wanao vaa nguo kma chatu wao huwa wanawahi pewa mafao yao kule psssf tofauti na washika chaki? tujiulize
Wale kule psssf wanajinadi na mfumo wanaotumia waliotoka nao PPF, data system zao zipo vizuri tho Challenges hazikosekani, ila mfumo wao wanaotumia umekaa vizuri michango inaingia na ni rahisi kufanya tracking.

Sasa NSSF wenzetu kule ukienda kuchukua fao lako ni mpaka waanze na kurekebisha michango wafuatilie michango ambayo haikuwekwa na mwajiri wako ndiyo mwanachama zianze process za kupewa pesa zake
 
Hao walio ndani kwa nyodo. Yaani hii dunia we acha tu. Unakuta mtu amefuata mafao ya ya laki tatu sasa wanavyo m treat.
Yote maisha aisee tena bora hilo ingia ofisi zao ndani sasa unakuta watu wanapiga story J3 asubuhi na njee reception unakuta kijana wa volunteer ndio anasaidia wazeee, shida sana hii.
 
Bado uwajibikaji serikalini ni mdgo sana, watu wanaishi kwa mazoea tu na sio kujituma kama zamani ndio shida hiyo.. Lakini kikubwa ni nidhamu hakuna... watu tunachukuliana poa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…