Nimeshangaa sana NSSF, asilimia kubwa wanaodai mafao ni vijana na si wazee kama ilivyokuwa zamani

Aiseeee!!!!!
 
Mimi Kuna jamaa zangu walizungushwa hivyo, ila walivyohonga tu mara mwingine laki nane,tisa mwingine M1 wakapata vibunda vyao

Ndiyo hivyo yani ukitaka msaada wa haraka na shortcut toa pesa upate pesa, sema siku hizi PCCB wanaingia kwenye mshirika haya wanawadakisha watumishi na pesa za moto,

Kuna jamaa wa malipo walimbeba inaonekana kuna mwanachama alimchomea, kwahiyo wana uoga kidogo siku hizi
 
Unashangaa nini sasa wakati kuna ukosefu wa ajira.
Mtu anasema Kwa nini usiendelee kufanya kazi 😳😤 akili za baadhi ya viumbe ni changamoto kwa kweli😤 kampuni/ taasisi/ shirika. Mtu alipokuwa anafanya kazi imefungwa ndio maana hana kazi, ndio maana mtu anaona heri achukue akiba yake imsaidie kipindi hiki lizamadamu linasema si ufanye kazi 🤷🏽‍♂️
 
Wajibu wa kufuatilia michango ya kila mwezi ni wa mfanyakazi, yaani mimi kila mwisho wa mwaka lazima niende kupata statement ya michango yangu na kama kuna inayomiss nafuatilia kazini na kuwapelekea Payslip ya mwezi unaomiss ili waingize.
 
Hasa kuna Kadada number 4 pale keupe ivi yani kanadharau sana chief
Napendaga sana wadada wenye dharau, mara nyingi huna naishia kuwala kiulainii... Mvumilie halafu tafuta weakness zake mkuu..
 
Kweli kweli ndiyo nashangaa vijana kushangaa mtu kukwapua ukwasi wake
 
Wajibu wa kufuatilia michango ya kila mwezi ni wa mfanyakazi, yaani mimi kila mwisho wa mwaka lazima niende kupata statement ya michango yangu na kama kuna inayomiss nafuatilia kazini na kuwapelekea Payslip ya mwezi unaomiss ili waingize.
Unachosema ni kweli kabisa, umejiwekea utaratibu mzuri sana na wa kimkakati, wengi hawajui kama wanatakiwa kufuatilia michango wenyewe wanasubiri mpaka mwajiri wao afanye hivyo
 
Ni kila taasisi
Hapana kiongozi. NSSF wamezidi. Siku ya kudai mafao utaambiwa.
1. Ujaze form x 3
2. Ulete bank statement x3
3. Ulete barua ya kuajiriwa x3
4. Ulete barua ya kuachishwa kazi x3 na certificate of service.
5. Ulete kadi ya NSSF
6. Ulete kadi ya NIDA
7. Ulete kadi ya CCM
8. Zile form zipigwe mhuri na mwajiri
9. Ulete picha tatu recent
10. Ulete kadi ya benki
11. Ulete barua toka benki ionyeshe kwamba kweli wewe ndio mmiliki wa hiyo account, iwekwe picha na mhuri wa benki uonekane.
12. Hivi vitu uvifanye ukiwa ushakaa jobless kwa kipindi. Sio unaachishwa leo halafu unajipendekeza kwenda NSSF.
13. Uwe mpole maana ukisharudisha hizo form, zinakaguliwa utafikiri unaingia gerezani, Kisha unasainishwa na kuambiwa uje baada ya miezi 2 waone Kama unastahili kulipwa au la. Kama hustahili unaambiwa uendelee kua mpole.
Ole wako, ole wako Kama unadai zaidi ya milioni tano halafu uonekane handsome/beautiful/msafi/unajiamini.
Utatafutiwa kosa kwamba mhuri fulani hauonekani vzr. Utarudishiwa form zako na kuanza upya.
Mimi nadhani kadi ya NSSF na kadi ya NIDA vinatosha na labda barua ya kuachishwa kazi.
Jiandaeni kisaikolojia kabla hamjaacha kazi.
Cha kushangaza NSSF Kuna watu wenye degree hata wenye master's wako wawili ninaowafahamu.
 
Ni kweli kabisa, mfano mzuri mimi nilipunguzwa kazini sababu ya Corona, nimejaza na kupeleka vitu vyote hivyo kasoro kadi ya CCM ndio sina, nikaambiwa nisubiri baada ya miezi miwili, lakini huu ni mwezi wa tatu sijaona chochote kwenye akaunti yangu.
 
Ni kweli kabisa, mfano mzuri mimi nilipunguzwa kazini sababu ya Corona, nimejaza na kupeleka vitu vyote hivyo kasoro kadi ya ccm ndio sina, nikaambiwa nisubiri baada ya miezi miwili, lakini huu ni mwezi wa tatu sijaona chochote kwenye akaunti yangu.
Na unaweza kusubiri hata kwa miaka 3, hawana utu kabisa wale jamaa.
 
Nchi imeoza kwa rushwa hii, kusoma tabu, ajira kuipata tabu, na bado kuchukua fao lako napo ni tabu tupu.
 
Ni kweli kabisa, mfano mzuri mimi nilipunguzwa kazini sababu ya Corona, nimejaza na kupeleka vitu vyote hivyo kasoro kadi ya ccm ndio sina, nikaambiwa nisubiri baada ya miezi miwili, lakini huu ni mwezi wa tatu sijaona chochote kwenye akaunti yangu.
Mwenyewe umekiri kadi ya CCM hujapeleka.
Aidha upeleke kadi ya CCM au gharama ya hiyo kadi ili wakuchukulie kwenye tawi lao kwa kukusaidia. Gharama ya hizi kadi adimu kwenye tawi lao Ni Kati ya sh ishirini na hamsini kutegemea na usumbufu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…