'Nimeshikwa, nashindwa kujinasua, hebu nisaidieni'

'Nimeshikwa, nashindwa kujinasua, hebu nisaidieni'

Dah!huyo kimada anaonesha kwanza hana adabu!anapata wapi courage ya kumpigia cm mke wa mtu?!afu mke wake anaonekana mvumilivu kweli!yan pamoja na yote hayo bado yupo tu!ushaur wa bure ni kwamba afadhal utulie na mkeo na mlee watoto!wanawake wa nje ni kama big G,utakosa vyote kaka!
 
Ungekua unampenda mke wako ungetulia tangu mwanzo na swala la kua na mke mwingine ungemhusisha kabla ya kujiweka kwenye mitego usiyoweza kuhimili.

Sasa you hav to deal with your mess...umeshajua kwamba kuendelea na mke wako inakubidi kuachana na huyo binti maana nyumba ndogo na mke mdogo vyote havikubaliwi na mke wako!!!Zaidi ya hapo ongeza unga uendelee kulikoroga mpaka liwe ugali alafu ushindwe kulinywa!!!

on a serious note Lizzy,sasa ndo umemshauri nini? Mwenzio anaomba advice,mpe.
 
Sijawahi ku comment Leo Mara ya kwanza. Sasa boss umeshindwa kuheshimu ndoa yako kwa ajili ya tamaa? Tumia akili watoto wako ni wakubwa. Uko tayari waone baba Yao kicheche. Achana na mambo ya ajabu in the name of utaoa mke wa pili. Kwani hata hiyo dini iliyoruhusu uoe wake watatu inataka masharti ya wewe kumheshimu mkeo. #nihayotu

Waminshari,waingereza wanasema 'you have hit the ground running',hongera kwa post yako!
 
We aha tu....

Uko wapi watu hapa wanakupa ushauri

MTM tupo ukurasa mmoja this dude was supposed to do better than this

How do you go all the way kumfahamisha mistress wako namba ya mkeo and the like

Hivi iyo 40K ulitoa kukiua kiumbe kisicho na hatia? Plus unamrudiaje mtu mwenye guts za kumpigia mkea na kumweleza maneno ya dharau kiasi hicho? Something must be seriously wrong...

We Acha Tu..REPENT.....nenda kwa mkea achana na hiyo ndito ya kimasai...mkeo hakuamini kwa sababy bado hujaonyesha kwa nini akuamini while unaendddelea na hako ka ndito...
 
Kaka heshimu ndoa yako,mche mola wako,onea huruma watoto wako.usitumie kivuli cha dini kuhalalisha"uzinzi" wako.
Watafta nini huko kwenye vyama vingi?
Ninachokiona hapa,wewe mwenyewe hupo tayari{willingness} kumuacha huyo kimada,sasa unataka tukushauri nini?angalia ucje ukawatesa watoto wako.mind u,mkeo akiondoka,c dhan km huyo kimada anaweza kulea watoto wako.kaka,wenzio twatafta wake walo tulia,wewe wachezea bahati hyo.duh!KWENYE MITI HAKUNA WAJENZI.
 
Tatizo siyo hawala, ila ni dhambi iliyopo moyoni mwako. YOU NEED JESUS,yeye ataiondoa dhambi inayokutesa.
 
kwa hyo unataka tukusaidiaje? Kama umenasa hebu jitikise tikise then ruka juu utakua ushajinasua.

Usitake kutusumbua vichwa kwa tamaa zako. siajabu umechuma na mkeo umepata vijisenti badala ya kutumia na familia yako unatapanya.
Mie namshauri mkeo atafte kiserengeti boy, maumivu utakayopata automatically huyo jini mla fedha wako aka hawara utamwacha mwenyewe.
 
unataka msaada gani hadi mtaa umehama mwenyewe kwa akili zako? pia unadai unawapenda wote mzinzi wewe.
mabadiliko ya mtu huwa yanafanywa na mtu mwenyewe jipange chukua hatuatubu acha uzinzi kimbia zinaa kama ulivomkimbia mkeo ukahamia mafichoni. acha tamaa
 
Hayo ndo matokeo ya kuwa na nyumba ndogo unajikuta unabomoa nyuma ya bati na kwenda kujenga ya nyasi, Rudi kikweli kikweli kwa mkeo na umuombe msameheane kadhalika mrudie Mungu wako kwa kutubia na kufanya mema na kuachana na hayo, usitake kuhalaisha tamaa kwa sheria za mungu. Tulia na mkeo mlee watoto wenu, vile vile kumbuka kucheki afya kama iko 100% OK.
 
Unaweza usiniamini haya niyaelezayo hapa, lakini ni ukweli mtupu na sasa sijui namna ambavyo ninaweza kutoka katika uhusiano huu maana sitaki kumkosesha raha mke wangu, ni kwamba mwaka 2007 niliingia kwenye mahusiano na binti mmoja aliyekuwa katika chuo kimoja mjini Morogoro wakati huo akiwa field Moshi kwenye moja ya taasisi ya serikali, basi nikatupa ndoano tukawa pamoja na hata aliporudi chuo kumaliza kozi yake.

mwaka mmoja baadaye alimaliza akarudi moshi akaanafanya kazi kwenye taasisi moja binafsi tutaka pamoja tena nilimtafutia chumba nikamweka huko nikawa mimi kama baba mwenye nyumba, siku moja tukiwa kwake tulikorofishana nikaondoka kwake nyumbani bila kuaga wakati naondoka njiani alinipigia simu sikupokea kama mara tano, nikazima simu. Nilipofika nyumbani akapiga simu ya mke wangu masikini alipokea tu, yule binti akasema 'Mwambie mume wako kesho anipe sh. 40,000 nikatoe mimba yake, nampigia simu yake ajidai kazima'.

Mungu wangu basi mke wangu kwa hekima akaniuliza "mumwe wangu haya aliyosema huyu dada ni kweli au naota? nikamuuliza amesema nini na ni nani? akasema kuna dada namba yake hii inafanana na yangu na yako (maana nilichonga namba zinazofafa zote zinatofautiana namba ya kwanza tu) anasema umpe hela kesho akatoe mimba yako.

Nikamwambie hebu tulale tuzungumze kesho mke wangu usiku huu ni mwingi tutagombana bure kwa ajili ya simu si unajua mitandao? nikajitetea na hoja yangu ikakubalika. Asubuhi ilipofika tukaanza mjadala lakini nilipojitetea alikubali lakini kadiri tulivyokwenda alizidi kubadilika mke wangu kutokana na fikra mpya zinavyomjia kutokana na maneno yale ya binti yule hata hivyo tuliendeleea hivyo hadi alipokutana naye yule binti baada ya kumfuata kazini kwake na kupigana naye.

Baada ya ugomvi huo mimi nikamwambia yule mwanamke nimemuacha karibu mara tatu na kweli nilimuacha kama miezi mitatu lakini baadaye nilirudi tena nikamuacha nikarudi tena nikamuacha nikarudi tena hadi leo hii tumehama sehemu ambayo mke wangu alipajua alipokuwa anaishi na sasa nimempangia chumba sehemu nyingine lakini mke wangu tangu alipogundua nipo na binti huyo haniamini tena kwani tangu nimemuoa mwaka 1997 hadi leo hakuwahi kuhisi nimetoka nje ya ndoa hadi tatizo hilo la binti huyo wa kimasai, sielewi nitatokaje na nimemwahidi kwamba nitamuo mke wa pili kwa vile mimi ni mwislamu lakini mke wangu hataki anasema nikimuoa huyo yeye anarudi kwao Tabora sasa nifanyeje?

Naomba mnishauri wote nawapenda mke wangu ambaye tuna watoto watatu mmoja ana umri wa miaka 14, wa pili 12 na wa tatu miaka minne na nusu. je nifanyeje?

yaani nimeimagne maumivu aliyoyapata mkeo mwili wote ukavibrate! Halafu unakuwaje na kimwanamke ambacho hakiwezi kustahimili mpaka kampigie mkeo simu eti peleka pesa akaue mtoto! Na ilikuwaje ukamchongea hawala namba inayofanana na ya mkeo? Ulizama sana eeh? Nachukia wasaliti jamani mie! Then Kwa usaliti huo nakushauri hv, kuwa gentleman, jiue wakukose wote!
 
Kwanza jitambue mwenyewe kuwa umri wako na matendo yako ni tofauti sana, upupu unaoufanya wa kumdharaulisha mkeo wa ndoa kwa hawara ni wa kitoto unafanywa hasa vijana wanaobalehe ndio wanakuwa na tabia ya kudharaulisha videm vyao kwa demu mpya,pili ni limbuken ambaye huoni thamani ya mkeo aliyekuvumilia ukiwa huna kitu na baada tu yakupata ukatafuta kimadatatu ww ni mwanaume usiyekuwa na haya hata kwa wanao wakubwa kwa kuendekeza uzinzi uliokosa heshima mpaka umri ulio nao,nne unajaribu kujastifai uzinzi wako kwa kutumia dini wakati hakuna dini inayoshabikia au kuruhusu uzinzi bila kufunga ndoa.
Ushauri wangu tubu dhambi zako kwa mkeo na wanao then mrudie mungu wako na utubu kweli,achana na huyo kimada kwani ukifulia tu huna chako kwake na kwa taarifa yako unasaidiwa na wenzio wengi tu ambao ni vijana wenzie na ukubali akilin na moyon mwako kwamba hakuna mwanamke mwingine dunian mzuri na anayekupenda km mkeo.
 
Sikiliza Mzab,asikubabaishe mtu hapa,unachokifanya wala sio cha ajabu,wanaume kibao (hata baadhi yao mamemba humu jf) wanafanya haya haya. Follow your heart bana maisha ni mafupi. Ka vipi bi mdogo we mzalishe kisha mjengee nyumba akuleleee mwanao. Huyo mkeo wala asikukondeshe haendi kokote,siku hizi hakuna mwanamke anaacha mwanaume,i am telling you!
 
Hujashikwa umejishikisha mwenyewe, kwanza tuambia kilichofanya ukaanza kutoka nje, mkeo mbaya, hakuridhishi ana matatizo ana mdomo? unapenda hayo mambo kwa sababu ungetaka kutoka ungetoka tangu siku ya kwanza mkeo alipogundua na usingerudi tena, halafu kwa mabinti wa nje inaonyesha unajua kuhonga ndo maana anakung'a n'gania ungekuwa choka mbaya wala asingetaka kuoana na wewe kuna cha ziada anapata. Na kwa taarifa yako ukishamuoa atakuambia umuache mke wako uwe na yeye peke yake. Utawatesa watoto wako hawana hatia kwa makosa yako, nimetoka kwenye familia ya baba wa dizaini yako watoto wa mama mkubwa ndo mara nyingi wanateseka na kama mama hatakuwa na juhudi atan'gan'gania kurudi Tabora, hao watoto wake hata shule hawataenda, maana wanawake wa pili huwa hawapendi watoto wa mke mkubwa wafanikiwe anaona watamsaidia mama yao wakiwa wakumbwa.

Kati ya makosa uliyowahi kufanya kwenye maisha yako ni hili. Pia omba Mungu sana shetani naye yupo kazini kuvuruga na kuharibu usimpe nafasi.
 
Sasa unataka tukushauri nini, mbona majibu umeshatoa kabisa, hiyo ndiyo inaitwa test the waters, then umekuta maji ya moto, kama Lizzy alivyosema u have to deal with ur mess!!!!!clean it up
 
yah kabisa cool, yani huyu guilty consciuos kwa mkewe ndiyo inayomtesa
 
Ndio maana mm napendelea wale wa kulipa, ku do na kuachana hapo hapo" for the betterment of my marriage"
 
Unaweza usiniamini haya niyaelezayo hapa, lakini ni ukweli mtupu na sasa sijui namna ambavyo ninaweza kutoka katika uhusiano huu maana sitaki kumkosesha raha mke wangu, ni kwamba mwaka 2007 niliingia kwenye mahusiano na binti mmoja aliyekuwa katika chuo kimoja mjini Morogoro wakati huo akiwa field Moshi kwenye moja ya taasisi ya serikali, basi nikatupa ndoano tukawa pamoja na hata aliporudi chuo kumaliza kozi yake.

mwaka mmoja baadaye alimaliza akarudi moshi akaanafanya kazi kwenye taasisi moja binafsi tutaka pamoja tena nilimtafutia chumba nikamweka huko nikawa mimi kama baba mwenye nyumba, siku moja tukiwa kwake tulikorofishana nikaondoka kwake nyumbani bila kuaga wakati naondoka njiani alinipigia simu sikupokea kama mara tano, nikazima simu. Nilipofika nyumbani akapiga simu ya mke wangu masikini alipokea tu, yule binti akasema 'Mwambie mume wako kesho anipe sh. 40,000 nikatoe mimba yake, nampigia simu yake ajidai kazima'.

Mungu wangu basi mke wangu kwa hekima akaniuliza "mumwe wangu haya aliyosema huyu dada ni kweli au naota? nikamuuliza amesema nini na ni nani? akasema kuna dada namba yake hii inafanana na yangu na yako (maana nilichonga namba zinazofafa zote zinatofautiana namba ya kwanza tu) anasema umpe hela kesho akatoe mimba yako.

Nikamwambie hebu tulale tuzungumze kesho mke wangu usiku huu ni mwingi tutagombana bure kwa ajili ya simu si unajua mitandao? nikajitetea na hoja yangu ikakubalika. Asubuhi ilipofika tukaanza mjadala lakini nilipojitetea alikubali lakini kadiri tulivyokwenda alizidi kubadilika mke wangu kutokana na fikra mpya zinavyomjia kutokana na maneno yale ya binti yule hata hivyo tuliendeleea hivyo hadi alipokutana naye yule binti baada ya kumfuata kazini kwake na kupigana naye.

Baada ya ugomvi huo mimi nikamwambia yule mwanamke nimemuacha karibu mara tatu na kweli nilimuacha kama miezi mitatu lakini baadaye nilirudi tena nikamuacha nikarudi tena nikamuacha nikarudi tena hadi leo hii tumehama sehemu ambayo mke wangu alipajua alipokuwa anaishi na sasa nimempangia chumba sehemu nyingine lakini mke wangu tangu alipogundua nipo na binti huyo haniamini tena kwani tangu nimemuoa mwaka 1997 hadi leo hakuwahi kuhisi nimetoka nje ya ndoa hadi tatizo hilo la binti huyo wa kimasai, sielewi nitatokaje na nimemwahidi kwamba nitamuo mke wa pili kwa vile mimi ni mwislamu lakini mke wangu hataki anasema nikimuoa huyo yeye anarudi kwao Tabora sasa nifanyeje?

Naomba mnishauri wote nawapenda mke wangu ambaye tuna watoto watatu mmoja ana umri wa miaka 14, wa pili 12 na wa tatu miaka minne na nusu. je nifanyeje?
Hadi sasa na ukae ukijua kuwa nawe una mume mwenza, na muda si mrefu utampata wa mwingine...! Kama hujaelwa ninachomaanisha, uje nikupigie hesabu hiyo uone...!
 
Wenye ndoa siku zote nawasihiii mtumie njia ya hit and run lakini nyinyi mnataka kujipumnzisha kabisa nyumba ndogo
 
Hadi sasa na ukae ukijua kuwa nawe una mume mwenza, na muda si mrefu utampata wa mwingine...! Kama hujaelwa ninachomaanisha, uje nikupigie hesabu hiyo uone...!

Aombe Mungu asipate kiserengeti boy maana kwanza atakuwa anakihonga huyo mke wake pili kitakuwa kinamrukisha ukuta
 
Back
Top Bottom