'Nimeshikwa, nashindwa kujinasua, hebu nisaidieni'

'Nimeshikwa, nashindwa kujinasua, hebu nisaidieni'

duh! hii kali.

sasa muheshimiwa hapa sasa itabidi tuu ukubali kuwa kunasehemu utachukiza ili ufuraishe upande mwingine.
kwa kuwa huyo demu sio mkewe..basi itabidi ukubali kurudi kwa mkeo na utulie nae. ila sasa nataka kukwambia kuwa ukisha amua kurudi na kukaa na mkeo basi wewe masisha yako yote utakuwa unajaribu kupata trust ya mkeo ambayo umeshaipoteza...... kiufupi umejifunga jela mara mbili!!!

umesema vyema,aachane na huyo mmasai,ajaribu kujenga mazingira yatakayorudisha uaminifu wake kwa mkewe
 
Kwanza kapime ujue status yako. Halafu kuanzia hapo uanze mikakati ya maisha mapya, maana hayo ya zamani inabidi uyaache yatakupeleka pabaya.
Hujasema kama mkeo mlikua na issues zozote zilizokufanya utoke nje, inaonekana hamna, so ni katabia tu. Hata ukimwoa huyo "mwisilamu mmasai" bado utatoka nje na mwingine. Badili tabia
 
Pole,
To be a true player you must know how to play
 
Lizzy huwa unanikonga moyo na point zako!
Huwa unawapa bila chenga.
Big up 😛oa

Hawa ndo walewale Lizy kuwa makini asije akakuPM akupangie chumba kama mzee mwenye thread hii.
 
We acha upuuzi unaofanya, hivi huyo mkeo unamchukuliaje, au unaona hana hisia wala uchungu anaoupata? Imagine kama ni yeye anakuambia anataka kuongeza mwanaume mwingine kwa sababu alimuahidi ataolewa naye. Naona unachezea hisia za mkeo, kesho naye akianza kukusaliti utadhubutu kumlalamikia? Hujui mambo ya mkuki kwa nguruwe? Acha upumbavu unaoufanya. Usitumie kigezo cha uislamu kicheza na hisia za mkeo, hata uislamu unamtaka mtu anayetaka kuongeza mke wa pili kuwasiliana na mke mkubwa na kukubaliana kuwa aoe mke wa pili, lakini si hiki unachokifanya ndugu, huo ni uzinzi tena ufirauni, na huo uufanyao ni umalaya, so we can call you malaya wa kiume. Nyambafu zako kabisa we mwanaume usieheshimu ndoa yako. '' ndoa na iheshimiwe na watu wote''
 
kaka pole,nadhani hilo ni fundisho kwa mimi na wanaumewote wakware.kaka achana nee huyo hawara yako,utakuja tesa watoto bure kwa ushenzi na tamaa zako zisizo kuwa na shukrani.utatia adabu.
 
Thanks Boss

Actually nilitaka kumshushia povu la karne huyo lofa

Yani wewe unacheat, ukishikwa unakimbilia JF?? Si kwamba mie ni msafi hapana, but madhara na tahadhari za cheating ziko wazi, so the dude knew exactly the risks associated

in addition, siamini kama mwanamke anaweza kupiga simu hivyo kama wewe hujamuonyesha kwamba unamdharau mkeo

IN MANY CASES NI SISI WANAUME TUNAOWADHARAULISHA WAKE ZETU KWENYE MECHI ZA UGENINI NA KUWAPA CONFIDENCE YA KUWEZA KUWADHARAU WAKE ZETU

USHAURI KWA MEMBER MWENYE POST 1.... JUST BE A MAN!![/QU Thank you.
 
wanaume kama nyinyi,mnafaa kuchunwa tu,maana hamna adabu

we kisukari weweeeeeee! yaani kuna wakati ukatoa maoni mazuri tu, ghafla unasema wanaume kama huyu wanafaa kuchunwa tu. Hivi jamani kisu hata kikiwa kikali vipi, kama kinakata nyama itafika wakati kitaisha makali na kuhitaji kunolewa. Inapofikiaga hapo kwenye kuisha makali na kuhitaji kunolewa ndipo unapokujaga utata kwa nyinyi kina dada.

Huwezi kumchuna mwanaume na wewe mwanamke ukabaki salama, kamwe hicho kitu hakipo jamani. If there is no win-win situation, basi lazima pawepo na loose-win situation. 'Ukipenda kuchuna basi uwe tayari kutumika' na katika hili 'wanaume wanajua kutumia'. Zinduka, Amka, Jifahamu na Chukua Hatua", vinginevyo.....................................'.
 
wakuu kama tumelewa ndumu au gongo/chang'aa ni vyema tulale
 
Si unataka kuoa mke wa pili eeh?? Oa baba oa uone watakavyokugawana kichwa!! Si unadhani ni kazi rahisi kuwahandle wote wawili pamoja na watoto?! FYI, hiyo kazi waliiweza wazee wetu tu na zama za p.o box ila kwa wakati huu wa capitalism na dot com baba utapumulia kisogo nakwambia!! Na ivi wa kwako wameonyesha kutopendana tangu awali (esp huyo nyumba ndogo) , majuto yake utaja simulia........wallah nakuapia!!
 
Sikiliza Mzab,asikubabaishe mtu hapa,unachokifanya wala sio cha ajabu,wanaume kibao (hata baadhi yao mamemba humu jf) wanafanya haya haya. Follow your heart bana maisha ni mafupi. Ka vipi bi mdogo we mzalishe kisha mjengee nyumba akuleleee mwanao. Huyo mkeo wala asikukondeshe haendi kokote,siku hizi hakuna mwanamke anaacha mwanaume,i am telling you!

Mdanganyeeeeeeeeeeee!!
 
Pole. Huna jinsi. Ongea vizuri na mke mkubwa ukimuomba radhi na kumweleza hali halisi ilivyo ukimuomba radhi akusamehe kwa dhambi ya uzinzi. Muombe akubali uoe mke wa pili kwa kuwa dini yako inaruhusu ila hukuwa mwaminifu tangu mwanzo. Akikataa kata kata, itabidi uachane na huyo binti.


Weeeeeeeeeeeeeee JASIRI HAACHI ASILI
 
Unaweza usiniamini haya niyaelezayo hapa, lakini ni ukweli mtupu na sasa sijui namna ambavyo ninaweza kutoka katika uhusiano huu maana sitaki kumkosesha raha mke wangu, ni kwamba mwaka 2007 niliingia kwenye mahusiano na binti mmoja aliyekuwa katika chuo kimoja mjini Morogoro wakati huo akiwa field Moshi kwenye moja ya taasisi ya serikali, basi nikatupa ndoano tukawa pamoja na hata aliporudi chuo kumaliza kozi yake.

mwaka mmoja baadaye alimaliza akarudi moshi akaanafanya kazi kwenye taasisi moja binafsi tutaka pamoja tena nilimtafutia chumba nikamweka huko nikawa mimi kama baba mwenye nyumba, siku moja tukiwa kwake tulikorofishana nikaondoka kwake nyumbani bila kuaga wakati naondoka njiani alinipigia simu sikupokea kama mara tano, nikazima simu. Nilipofika nyumbani akapiga simu ya mke wangu masikini alipokea tu, yule binti akasema 'Mwambie mume wako kesho anipe sh. 40,000 nikatoe mimba yake, nampigia simu yake ajidai kazima'.

Mungu wangu basi mke wangu kwa hekima akaniuliza "mumwe wangu haya aliyosema huyu dada ni kweli au naota? nikamuuliza amesema nini na ni nani? akasema kuna dada namba yake hii inafanana na yangu na yako (maana nilichonga namba zinazofafa zote zinatofautiana namba ya kwanza tu) anasema umpe hela kesho akatoe mimba yako.

Nikamwambie hebu tulale tuzungumze kesho mke wangu usiku huu ni mwingi tutagombana bure kwa ajili ya simu si unajua mitandao? nikajitetea na hoja yangu ikakubalika. Asubuhi ilipofika tukaanza mjadala lakini nilipojitetea alikubali lakini kadiri tulivyokwenda alizidi kubadilika mke wangu kutokana na fikra mpya zinavyomjia kutokana na maneno yale ya binti yule hata hivyo tuliendeleea hivyo hadi alipokutana naye yule binti baada ya kumfuata kazini kwake na kupigana naye.

Baada ya ugomvi huo mimi nikamwambia yule mwanamke nimemuacha karibu mara tatu na kweli nilimuacha kama miezi mitatu lakini baadaye nilirudi tena nikamuacha nikarudi tena nikamuacha nikarudi tena hadi leo hii tumehama sehemu ambayo mke wangu alipajua alipokuwa anaishi na sasa nimempangia chumba sehemu nyingine lakini mke wangu tangu alipogundua nipo na binti huyo haniamini tena kwani tangu nimemuoa mwaka 1997 hadi leo hakuwahi kuhisi nimetoka nje ya ndoa hadi tatizo hilo la binti huyo wa kimasai, sielewi nitatokaje na nimemwahidi kwamba nitamuo mke wa pili kwa vile mimi ni mwislamu lakini mke wangu hataki anasema nikimuoa huyo yeye anarudi kwao Tabora sasa nifanyeje?

Naomba mnishauri wote nawapenda mke wangu ambaye tuna watoto watatu mmoja ana umri wa miaka 14, wa pili 12 na wa tatu miaka minne na nusu. je nifanyeje?

Mm naokupa pole maana kosa si lako bali, kosa ni la sera potofu, zisizotekelezeka zilizoletwa na mtume salaula mohammad, kwamba wamaume wanaweza kuoa mke zaidi ya mmoja!
 
Back
Top Bottom