...hivi sasa napoongea shemeji keshahama hostel anaishi kwa jamaa, wanapika na kupakua.
Hicho kitu kimeniumiza sana hasa ukifikiria ni mke wa rafiki yangu. Kwasababu alijua anachokifanya, shemeji sasa ananionea aibu sana kiasi kwamba hata nikimpigia simu hapokei. Wakati naendelea kutafakari nini cha kufanya, nikapokea simu kutoka kwa huyo rafiki yangu (mwenye mke) akinituhumu kuwa mkewe kampigia simu kuwa mimi nimemtongoza na nataka niwe na mahusiano naye kimapenzi, kwakuwa jamaa anamuamini sana mkewe na anampenda mno, amefedheheshwa sana na taarifa hizo hasa ukizingatia sisi ni marafiki wa siku nyingi, jamaa ameapa kunichinja siku tukionana. Nimejaribu kumuelewesha jamaa haelewi.
Wandugu nifanyeje?
(Samahani sana kwa kuweka stori ndeeeefu lakini ilibidi nifanye hivi ili issue iwe clear kidogo)