Nimeshindwa biashara

Nimeshindwa biashara

mwalidebe

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2016
Posts
425
Reaction score
250
Mimi nimekuwa nikifanya biashara muda mrefu,nataka kuachana na biashara ili niangalie mambo mengine. Sasa nawezaje kuachana na hii leseni ya biashara na tini namba?
 
Rahisi tu, ukifika sea view pale tupa madocument yote chini ya daraja
 
Mkuu ulikua unafanya biashara gani? Nini sababu iliyopelekea wewe kushindwa biashara?
 
Kila siku tunahimizwa humu tuanzishe bzness. Imekuwaje Tena?
 
Mimi nimekuwa nikifanya biashara muda mrefu,nataka kuachana na biashara ili niangalie mambo mengine. Sasa nawezaje kuachana na hii leseni ya biashara na tini namba?
Waandikie barua mamlaka husika kuhusu kusitisha biashara,ili wakuondoe kwenye kodi
 
Kwa ushauri usifunge biashara;'mjasiriamali hafungi biashara bali anapambana nayo mpaka inasimama,ila mfanyabiashara anayumbishwa na mabadiliko ya mauzo' kama wewe ni mjasiriamali pambana,na kama wewe ni mfanyabiashara endelea na uamuzi wako.
 
Kweli maisha yamebadirika sana mimi nataka niache ufundi nifanye biashara wewe unataka kuacha biashara ufanye nini tutakimbilia wapi kwa hali hii inavyozidi kuwa tete
Ku-maintain biashara ikasimama siyo jambo dogo hata kidogo.biashara inataka uvumilivu na kujituma ukifanya biashara kwa mazoeya utafunga!

Hasa awamu hii wale waliokuwa wamezoea kipindi cha white kufunga hesabu jioni million 5 kwenda juu wameingia wenge hatari,unakuta mtu mpaka jioni kwenye draw mna 800K hajalipa wafanyakazi hajachukuwa hela ya mafuta hao lazima wakimbie.

Ila kwa utawala huu kama utaweza kuanzisha biashara ikasimama basi kuja kudondoka itakuwa kazi sana maybe uwe tu na kichwa kibovu.
 
Habari mbaya hii, sikushauri uache kabisa bali ufanye mabadiliko ya ufanyaji wa biashara yako.

Andika barua yenye kichwa kisemacho KUFUNGA BIASHARA, maudhui yake yawe ni sababu zinazokufanya usiendelee na biashara husika, ipeleke TRA watakuelekeza zaidi.

Unaweza funga hiyo ukafungua biashara ndogo isiyolipiwa kodi wala haihitaji leseni a.k.a biashara za barabarani au umachinga ili ujijenge upya.
 
Kwa ushauri usifunge biashara;'mjasiriamali hafungi biashara bali anapambana nayo mpaka inasimama,ila mfanyabiashara anayumbishwa na mabadiliko ya mauzo' kama wewe ni mjasiriamali pambana,na kama wewe ni mfanyabiashara endelea na uamuzi wako.
Sio kila MTU amezaliwa kufanya biashara wengine wamezaliwa kuwafanyia kazi wenzao..mwache aende alipopachagua..
 
Back
Top Bottom