Kuna UPUMBAVU umewaganda watu ambao Hupenda kusema eti kuacha kamari haiwezekani. Am telling you, hizi ni kauli za kipepo. Just Fanya maamuzi ya kutoka kama ulivyofanya maamuzi ya kuingia.
Huwezi kuacha kamari kwa kupewa ushauri na wacheza kamari. Amua kuamua na uieleze kamari kuwa Leo ndio ndoa yetu imefika mwisho.
Amua, maanisha, na tafuta Jambo mbadala la kujiburudisha.
Kwanza ujue kamari sio burudan ni biashara.
Pili usilinganishe pesa ya pombe au malaya na ya kamari maana ya kamari unafukuzia kitu kikubwa mno cha faida na pombe ni unatumia mazma au kuteketeza mazma hicho ulichopata. Plus na sumu mwilini.
Ukamaria misingi yake ni tamaa ya kupata haraka!
Ndio maana wakamaria pia ni wahangaikaj sana. Roho zina ombwe kubwa na ugomvi kati ya matamanio yao vs uwezo wao.
Ukamaria wa mikeka kwa wanaojua wanachofanya na kanuni zake ni biashara kama nyingine.
Kuhusu kuacha mdau aanzie na kamari ya mechi tu.
Na hata asiende casino kujua kinachojiri.
Asijari hata connections zinazoanzia casino.
Abadiri aina ya marafiki ili kubadiri story za maisha.
Apende kupatikana nyumba za ibada (zisizo na makelele) au msikitin.
Apende kusoma vitabu vya maarifa hasa aina kadhaa za uwekezeji wa kuwa milionea.
Apende kufanya mazungumzo na watu wenye falsafa kiwango cha juu kama Dr Ellie.
Watu wa kuombea sana ni wakamaria wa casino kama huyu mdau na wakamaria wa virtual games na machine za wachina.(Anything programmed). Huko ndo utakutana na msemo wa .THE HOUSE ALWAYS WINS!
(mpaka sasa watu pekee wanaofaidika kwa mcheza kamari ni wake maana mcheza kamari hajawai kukimbizana na ratba za kuchepuka maana hawana nguv za kiume, ni jamii ya mateja. hadi wakila ndo kwa mbaaali....)