mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,925
- 51,688
Baba yangu mzazi alihamia Dar es salaan mwaka 1968, akiwa kijana,
Tangu miaka hiyo mpaka anazeeka alienda kwao nara chache sana,niseme tu hakupapenda kwao,maana hakujenga hata slope kule kijijini.
Siku zote alikuwa akisema akifa azikwe hukuhuku mjini,manispaa ya ubungo kuanzia kimara mpaka kibamba walikuwa wanazika tu nyumbani kama una eneo kubwa.
Korona ya nwaka 2021 ikaondoka na mzee,tukafuatilia kibali cha mazishi ili tumzike nyumbani,wakatukatalia wakisena huu sasa ni mji na ni manispaa japo aliacha eneo kubwa tu,tukaenda kumzika makaburi ya umma.
Pembeni yake palikuwa wazi nikapalipia ili nikifa nizikwe karibu na mzee maana mi sina kwetu?
Hiki ni kitu cha kawaida sana,wengi wanaozikwa kinondoni cemetry walishalipia site zao kitambo,kwa ufupi pameshajaa kabla ya kujaa,sio kitu kipya,mji unakua na maeneo ya kuzikia hakuna. Chimbo jipya sasa kwa wakazi wa jimbo la kawe na maeneo jirani ni makaburi ya kondo.
Turudi kwenye mada,sasa mwaka jana nikakuta site yangu kuna kaburi jipya,Nikaanza fujo fujo mpaka baraza la usuluhishi la kata.
kufuatilia nyaraka sijalipia ada ya mwaka 2022 ada ndogo tu ya 10000 kila mwaka.huwa wanaweka ada ya kila nwaka kama kuhakiki kuwa huyu mmiliki yupo hai au alishajufa,badhani hata NSSF wana huo utaratibu wa kulipa mafao baada ya uhakiki.
Wananzengo ndio hivyo nimeshakosa haki yangu nikifa nizikeni popotetu.