Uchaguzi 2020 Nimeshindwa kuwachangia makamanda, niliitupa line ya Voda

Hapo ndio hata mm nashangaa, na hii imepelekea kushindwa kupata pesa kwa baadhi ya watu
 
Ni kweli juzi hali yangu ilikuwa mbaya, ila jana na leo kuna mishe nimefanya nimepata pesa ila nashindaa kuchangia
 
Debe tupu haliachi kupiga kelele, Kama mtu anataka kuchangia jambo atahakikisha anachangia tu sababu atoaye hutoa katika hazina yake.
Kwa sisi ambao hatuna mpesa au tigo pesa au airtel money tunachangiaje?
 
Hata Tigo-pesa inashindikana. Nimejaribu mara kadhaa pesa inarudishwa. Ninyi viongozi wetu mtuambie la kufanya. Tunapenda sana kuchangia kampeni za CHADEMA.
Afadhali wewe una tigo pesa, sisi wengine wenye halo pesa tumetengwa.
 
Kupingana na ulichokiongea ndio tabia ya wanasiasa, Rais Magufuli alisema kwenye serikali yake ukiharibu ndio byebye lakini Anne Kilango Malecela aliharibu kwenye ukuu wa mkoa tena akamdanganya rais na bado akapewa ubunge
 
Unakumbuka fedha zilizozuiwa bank na polisi zilizotoka nje kupitia NGO moja?
 
Wewe kila siku na michango tu, huna habari nyingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…