Kasheshe.
Hicho si kitu cha kushangaa hata kidogo kwa sababu hata hapa First World USA watu wanakesha hata siku 7 kusuburi matokeo ya kura.
Kuchakachua kura kupo kila mahali. Wenzetu hawa walio dunia ya kwanza nao ni wachakachuaji wa kura tunachotofautiana ni Technolojia ya kuchakachua.
Wenzetu zaidi ya upigaji kura huu wa kawaida pia wana Electronics Voting Machines, wakati wa kuprogram software kuna mamluki kadhaa wamejaribu kuprogram ili jambo fulani lisilo kusudiwa litokee kwa manufaa ya kundi fulani.
kulinda karatasi ya kura yako ni muhimu aidha kulinda uchakatuaji wa matokeo baada ya kupiga kura ni muhimu pia.
Mpaka niongeapo bado haijagundulika Technolojia kali ya ulinzi zaidi ya ile ya kuweka kiwngu cha watu wakiwa na nyusu kakamavu na macho makali kama miali kuhakikisha jambo baya halitokei dhidi Lindo lao.
Teknolojia popular,ya kulinda usalama mahali pengi ikiwa ni pamoja na uchakachuaji ,hapa first World ni kulinda kwa kutumia Video Camera jambo tutakalo lifanya 2015. Hata hivyo ulinzi huo unahitaji watu kadhaa kuwapo Control Room 24/7 wakiwa macho bila kumbonji other wise Technolojia inabakia kuwa ni upuuzi fulani.Hii Technolojia ya kulinda kura kwa Video lazima ije baada ya kufanya mabadiriko makubwa ya Katiba yenye baadhi ya sheria za kidikteta, kiimla na kisultani.
Hata hivyo ni ukweli usiopingika kwamba watu hawana kazi na hili si jambo la mchezo mchezo kwa mtu yeyote au chama.
Idadi ya watu wasio kuwa na kazi ikiongezeka ni hatari kwa stability ya kisiasa. Tena ni hatari zaidi iwapo vijana wasio na kazi ni kundi la wasomi. CCM ndiyo waliotufikisha hapa kwa makusudi kabisa na wana nia ya kutupeleka kubaya zaidi. sijui nia madhumuni na makusudio yao ni nini?
Sehemu nyingi sana nchini Tanzania,Imani kwa vyombo vya kiserikali imezidi kupungua na si muda mrefu sana ujao itatoweka kabisa kama utawala wa CCM utadumishwa kwa mabavu.
Katika siku za hivi karibuni sisi wananchi tumeanza kutilia mashaka mwenendo wa viongozi wa juu wa JWTZ kutoka na matamshi yao tata. Viongozi wa juu wa JWTZ kutoa matamshi yenye ushabiki wa kisiasa ni sawa kabisa na kufanya mapinduzi haramu kupitia mgongo wa CCM.
JWTZ ndiyo wenye Bunduki Risasi Vifaru Mizinga Mabomu ya kila namna na ujuzi na uwezo wa kutekeleza jambo kwa nguvu na lazima. Uwezo huo tumewapa ili walinde maadui kutoka nje ya nchi hii wasije wakachukua sehemu ya ardhi au nchi yote kwa ujumla. Matamshi ya hivi karibuni ya Afande Shimbo ni dalili moja kubwa kwamba jeshi limesahau wajibu wake wa kuelekeza mtutu kwa madui wa nchi na kuanza kuuelekeza kwetu sisi wananchi kwa manufaa ya Mafisadi wa CCM mabao hawaachi kuwamegea ngawira haramu za ufisadi.
JWTZ hawatakiwi kujiingiza katika mambo ya upigaji kura kufanya hivyo ni kinyume cha katiba ya Jamhuri ya Tanzania.
Maadui wa Jamhuri ndani yanchi wanashughulikiwa na POLISI.
Upinzani wa kisiasa si Vita wala si kosa la Jinai Kwa hiyo hata POLISI hawatakiwai kuviona vyama vingine visivyo kuwa madarakani kama ni makundi ya wahalifu.
Polisi wakiegemea upande mmoja au kwa kutii amri haramu za wakuu wao au kwa kujipendekeza kwa wanasiasa au kwa kutaka kunufaika kwa namna yeyote. Wananchi wa Tanzania wana haki ya kikatiba ya kujitolea muhanga kulinda haki zao zisifinyangwe na Mamrki wa kisiasa.
Haki yako ikiisha kuchezewa kwa muda mrefu inakuplelekea kung'amua kwamba mlinzi namba moja na muhimu ni wewe mwenyewe.