Melezo yako ni magumu kukuelewa. Ulinunua gari na hukuwa kulipa deni (inavyoonekana miaka mitano au zaidi iliyopita kama nitakuwa nimekuelewa vizuri). Halafu ukaliuza au ukahamisha milki kwa mtu mwingine kinyume cha sheria maana hukuwa na hata milki kwa kuwa huna kadi halisi ya gari (original Card). Nakama nimekuelewa pamoja na kuliuza gari ilo hukutaka kumaliza deni ili upewe kadi na kufanya uhamisho kisheria.
Ki ukweli una kazi kujitetea maana hukutaka kuhalalisha umilki wa gari kumbe gari la wizi na nadhani wamekushitaki kwa kukutwa unamilki mali ya wizi Kisheria inaitwa (possession of stolen property) ambalo ni kosa la jinai