Tundu Lissu kupitia akaunti yake ya mtandao wa X amewachochea Wamasai wa Ngorongoro wasihame kwa hiari kwenda Msomera, Handeni. Nimeshtushwa mno!
Nimejiuliza, Lissu ni katili hivi kumbe? Kumbe Lissu ni adui wa ndugu zetu Watanzania wa jamii ya Wamasai? Kwa sababu wahenga wanasema adui yako mwombee njaa! Lissu anawaombea njaa na dhiki Wamasai.
Tupime hoja; ndugu zetu Wamasai wanaohama kwa hiari kwenda Msomera wanapewa na serikali utajiri ufuatao:
(i) Eneo la ekari 2.5 za ardhi lenye nyumba moja, choo na bafu za nje.
(ii) Ekari tano za ardhi kwa ajili ya kilimo.
(iii) Wanapewa hatimiliki za ardhi hiyo.
(iv) Kuunganishwa miundombinu ya umeme na eneo la malisho.
Pia soma: Wamasai Ngorongoro wamechoka kunyang’anywa ardhi yao na kupewa Mwarabu, Wameamua liwalo na liwe
Huu ni utajiri mkubwa. Mmasai huyu baada ya miaka 10 thamani ya utajri wake kutokana na mali ardhi na nyumba alizopewa na serikali utakuwa mkubwa.
Waliowahi kupewa maeneo ya Kigamboni enzi za Mwalimu Nyerere wanajua thamani ya kinachofanywa na serikali kwa Watanzania wa jamii ya Kimasai , waliokataa wanajuta. Leo hii huwezi kupata ardhi kwa bei rahisi Kibugumo, Gezaulole maarufu kama Geza wala Mwanagilato Kigamboni.
Pili, Lissu anajua azma ya serikali kwa kushirikiana na jamii ya Kimasai ni kulinda Hifadhi ya Ngorongoro, kwani ni urithi wetu wa dunia unaotambuliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO).
Tatu, Lissu anajua utalii ni chanzo kikubwa cha kuingizia serikali fedha za kigeni. Lissu hataki Tanzania ipate fedha za kigeni ili tutegemee wajomba zake wa Ulaya!
Nne, nimeamini Lissu ni mamluki mzuri anayeweza kujilipua kwa maslahi ya maadui wa Taifa letu. Lissu hajawahi kusimama upande wa serikali Serikali dhidi ya vita ya uchumi. Amekuwa silaha ya kukodi.
Kumbe Lissu anatumika na Amnesty International, Human Rights Watch na baadhi ya majirani kuhujumu utalii na kutaka kuivuruga nchi yetu nzuri.
#Lissu must go kwenye siasa za Tanzania, ni mamluki hatari anayejidai mzalendo.