Nimeshuhudia aisee Kilimo kinalipa sana

Kilimo kinalipa sana ila shida soko ndo tatizo kabisa. Leo nimepita sokoni nyanya tenga kwa mchuuzi linauzwa 32000 debe mbili je mkulima kauzaje? Nikifikiria hapo huwa naona bora nikazane kilimo cha miti
Mkuu nafikiri ili kilimo kikunufaishe unapaswa kuwa na target ya soko lako. Hiyo hiyo nyanya ukilima sasa hivi na ukauza mwezi wa 1 itakulipa sana. Kilimo ni sayansi mkuu
 
Mkoa wa singida boss
 
Nadhani kanuni za kimungu za mafanikio zinaweza kunisaidia. Asante mkuu
 
Wna
 
Kwanza nikupongeze kwa udadisi wa kutaka kujua jinsi ya kupata mafanikio.
Lakini bado kwenye udadisi wako umebakisha vitu viwili ili ukamilike na kupata conclusion kuhusu kilimo.
1.Ungewauliza hayo maendeleo uliyoyaona kwa hao jamaa zako walitumia miaka mingapi Hadi kufanikiwa.
2.Ukaanze kulima kwa misimu miwili au mitatu mfululizo baada ya hapo utakuwa umepata uzoefu wa kilimo kuanzia maandalizi ya shamba,kupanda,palizi,kuvuna,kutafuta masoko na kuuza.
Halaf baada ya hapo utuletee mrejesho ili na sisi ikiwezekana tufuate nyayo zako.
 
Ukijaribu ndiyo utajua ugumu na urahisi wake...

Kama wao walivyoshindwa kuendelea na masomo ila wewe ukaweza... nawe ukiingia kwenye sector kama yao unaweza angukia pua...


Cc: mahondaw
 
Wapi huko mkuu maana umenitamanisha
 
Mkuu
Kuna kitu nimejifunza katika maisha kwanza Usione ukadhani na Usichukulie kila kitu at face value.Kilimo kweli kinalipa na elimu pia inalipa.Kati ya wasomi kuna waliotusua na waliotusuliwa na kati ya wakulima kuna waliotusua na waliotusuliwa.

Kwa ufupi nakushauri unywe maji the utuli utafakari kwa kina.
 
Je unahitaji kulima mahindi na hauna muda wa kusimamia? Au unataka upate mavuno mengi zaidi? Njoo ofisini kwetu.

Ofisi ya YAD yenye wataalamu wabobezi wa kilimo sasa inakuletea mpango wa kusimamia shughuli zote za shambani. Mkulima utatukabidhi shughuli zako pale shambani kwako sisi tutafanya kila kitu kwa utaalamu zaidi na kukukabidhi mazao yako yakiwa yamekomaa. Gharama zetu ni nafuu sana na tunakuhakikishia kwa ekari moja kuvuna mahindi zaidi ya gunia 30. Usihangaike sasa, sisi tupo kwa ajili yako, Kwa Wale ambao hawana mashamba tutakuwezesha kupata mashamba ya kukodi kwa elfu 40 tu na mashamba ya kununua kwa elfu 60 tu hata ukihitaji ekari 100 za kununua utazipata kwa bei hiyo hiyo.

Kwa maelezo zaidi fika ofisini kwetu.
Jengo la NSSF SONGEA
Ghorofa ya 3 chumba no. 317
Simu. 0621133117
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…