Nimeshuhudia aisee Kilimo kinalipa sana

Nimeshuhudia aisee Kilimo kinalipa sana

Kilimo kinalipa sana ila shida soko ndo tatizo kabisa. Leo nimepita sokoni nyanya tenga kwa mchuuzi linauzwa 32000 debe mbili je mkulima kauzaje? Nikifikiria hapo huwa naona bora nikazane kilimo cha miti
Mkuu nafikiri ili kilimo kikunufaishe unapaswa kuwa na target ya soko lako. Hiyo hiyo nyanya ukilima sasa hivi na ukauza mwezi wa 1 itakulipa sana. Kilimo ni sayansi mkuu
 
Huko kwenu kuna neema, hicho sio kijiji tena kushakuwa mji kama noah, bodaboda, majumba makali yamejazana hivyo. Huku kwetu jembe la mkono halilipi kuna kipindi hali inakuwa mbaya zaidi ukiwa na elfu kumi wewe tajiri. Kilimo kisikie hvhv.
Mkoa gani huo niwashitue wana tuzamie huko.
Mkoa wa singida boss
 
Kila kitu kinalipa kama mtu anaweza kuutumia ulimwengu wa roho kukifanikisha, sasa muone mtu aliyefanikiwa kwa kutumia ulimwengu wa roho Halafu wewe usiutumie uone matokeo?!

Ulimwengu wa roho ni:

- ushirikina
- kanuni za ki Mungu za mafanikio!

Mshana Jr - Upo Kaka?
Nadhani kanuni za kimungu za mafanikio zinaweza kunisaidia. Asante mkuu
 
Wna
Mkuu wanalima kilimo gani huko? All in all acha kilimo cha kwenye madaftari end of the day utalia na kusaga meno
[/QUOTE
Wanalima mahindi alizeti maharage na dengu. Kilimo cha kwenye makaratasi nilikuaga nacho zamani ila nilipoingiaga field nikaona mambo ni tofauti kabisa. Siku hizi nalima kilimo cha shambani
 
Kwa wiki nzima sasa nimezunguka vijiji kadhaa nikifanya ziara ya kitafiti kuhusu kilimo. In fact tusiite ziara niseme tu nachunguzachunguza mustakabali wa kilimo kupitia kivuli cha kuwatembelea ndugu zangu wajomba na mashangazi vijijini huko ndani ndani.

Asikuambie mtu kilimo kinalipa. Majority ya wakazi wa kijijini niliofanikiwa kukutana nao wanalima small scale agriculture kwa kutumia jembe la mkono na ni kilimo local sana.

Ajabu ni kwamba watu wanaendesha maisha yao vizuri kabisa. Kuna vijana wa rika langu ambao wakati mimi nafaulu vizuri na kuendelea na elimu ya sekondari, wao hawakubahatika hivo wakalazimika kubaki kijijini kulima.

Leo nimekutana nao wana maisha mazuri kwelikweli. Wote wamejenga nyumba zao. Unaweza kusema kujenga kijijini sio gharama kubwa. Lakini hawa vijana wametumia tofali za block kama mjini, nyumba zao zina dirisha za aluminium na wengine tiles kabisa. Vijana wengine kadhaa wamemiliki gari zao nzuri tu kama Toyota Noah na malori. Bodaboda ndo usiseme zipo nyingi.

Kuna jamaa mmoja tulisomaga naye shule ya msingi alikua kilaza kweli. Karibia kila mtihani alikua wa mwisho. Ni mtu aliyedharaulika mno. Leo nikakutana naye dukani kwake tukawa tunapiga stori. Ana mke na watoto. Amejenga nyumba nzuri. Pia ana Toyota Noah namba D mpya kabisa rangi nyeusi. Akaniambia mafanikio yote hayo ni kilimo na analima kilimo cha kienyeji. Sasa mimi niliyekuwa masomoni nikijiangalia sina hela naona aibu japo inashauriwa usijilinganishe na mtu bali jilinganishe wewe wa jana na wewe wa leo.

Sasa nimekaa nikatafakari kama hawa wakulima wa kienyeji wanapiga hela hivi, vipi akienda mtu alime maeneo yale yale kwa kilimo chenye tija? Alime kwa kufuata taratibu zote za kilimo? Si atatoboa upesi sana?

Wakulima wazoefu mkuje huku kutuambia kama kilimo kinalipa au la. Maana nilichokiona leo kimenitia nguvu sana nikalime.
Kwanza nikupongeze kwa udadisi wa kutaka kujua jinsi ya kupata mafanikio.
Lakini bado kwenye udadisi wako umebakisha vitu viwili ili ukamilike na kupata conclusion kuhusu kilimo.
1.Ungewauliza hayo maendeleo uliyoyaona kwa hao jamaa zako walitumia miaka mingapi Hadi kufanikiwa.
2.Ukaanze kulima kwa misimu miwili au mitatu mfululizo baada ya hapo utakuwa umepata uzoefu wa kilimo kuanzia maandalizi ya shamba,kupanda,palizi,kuvuna,kutafuta masoko na kuuza.
Halaf baada ya hapo utuletee mrejesho ili na sisi ikiwezekana tufuate nyayo zako.
 
Ukijaribu ndiyo utajua ugumu na urahisi wake...

Kama wao walivyoshindwa kuendelea na masomo ila wewe ukaweza... nawe ukiingia kwenye sector kama yao unaweza angukia pua...

Cc: mahondaw
 
Kwa wiki nzima sasa nimezunguka vijiji kadhaa nikifanya ziara ya kitafiti kuhusu kilimo. In fact tusiite ziara niseme tu nachunguzachunguza mustakabali wa kilimo kupitia kivuli cha kuwatembelea ndugu zangu wajomba na mashangazi vijijini huko ndani ndani.

Asikuambie mtu kilimo kinalipa. Majority ya wakazi wa kijijini niliofanikiwa kukutana nao wanalima small scale agriculture kwa kutumia jembe la mkono na ni kilimo local sana.

Ajabu ni kwamba watu wanaendesha maisha yao vizuri kabisa. Kuna vijana wa rika langu ambao wakati mimi nafaulu vizuri na kuendelea na elimu ya sekondari, wao hawakubahatika hivo wakalazimika kubaki kijijini kulima.

Leo nimekutana nao wana maisha mazuri kwelikweli. Wote wamejenga nyumba zao. Unaweza kusema kujenga kijijini sio gharama kubwa. Lakini hawa vijana wametumia tofali za block kama mjini, nyumba zao zina dirisha za aluminium na wengine tiles kabisa. Vijana wengine kadhaa wamemiliki gari zao nzuri tu kama Toyota Noah na malori. Bodaboda ndo usiseme zipo nyingi.

Kuna jamaa mmoja tulisomaga naye shule ya msingi alikua kilaza kweli. Karibia kila mtihani alikua wa mwisho. Ni mtu aliyedharaulika mno. Leo nikakutana naye dukani kwake tukawa tunapiga stori. Ana mke na watoto. Amejenga nyumba nzuri. Pia ana Toyota Noah namba D mpya kabisa rangi nyeusi. Akaniambia mafanikio yote hayo ni kilimo na analima kilimo cha kienyeji. Sasa mimi niliyekuwa masomoni nikijiangalia sina hela naona aibu japo inashauriwa usijilinganishe na mtu bali jilinganishe wewe wa jana na wewe wa leo.

Sasa nimekaa nikatafakari kama hawa wakulima wa kienyeji wanapiga hela hivi, vipi akienda mtu alime maeneo yale yale kwa kilimo chenye tija? Alime kwa kufuata taratibu zote za kilimo? Si atatoboa upesi sana?

Wakulima wazoefu mkuje huku kutuambia kama kilimo kinalipa au la. Maana nilichokiona leo kimenitia nguvu sana nikalime.
Wapi huko mkuu maana umenitamanisha
 
Mkuu
Kuna kitu nimejifunza katika maisha kwanza Usione ukadhani na Usichukulie kila kitu at face value.Kilimo kweli kinalipa na elimu pia inalipa.Kati ya wasomi kuna waliotusua na waliotusuliwa na kati ya wakulima kuna waliotusua na waliotusuliwa.

Kwa ufupi nakushauri unywe maji the utuli utafakari kwa kina.
 
Je unahitaji kulima mahindi na hauna muda wa kusimamia? Au unataka upate mavuno mengi zaidi? Njoo ofisini kwetu.

Ofisi ya YAD yenye wataalamu wabobezi wa kilimo sasa inakuletea mpango wa kusimamia shughuli zote za shambani. Mkulima utatukabidhi shughuli zako pale shambani kwako sisi tutafanya kila kitu kwa utaalamu zaidi na kukukabidhi mazao yako yakiwa yamekomaa. Gharama zetu ni nafuu sana na tunakuhakikishia kwa ekari moja kuvuna mahindi zaidi ya gunia 30. Usihangaike sasa, sisi tupo kwa ajili yako, Kwa Wale ambao hawana mashamba tutakuwezesha kupata mashamba ya kukodi kwa elfu 40 tu na mashamba ya kununua kwa elfu 60 tu hata ukihitaji ekari 100 za kununua utazipata kwa bei hiyo hiyo.

Kwa maelezo zaidi fika ofisini kwetu.
Jengo la NSSF SONGEA
Ghorofa ya 3 chumba no. 317
Simu. 0621133117
 
Back
Top Bottom