SNAP J
JF-Expert Member
- Dec 26, 2013
- 7,106
- 8,043
Nilikuwa nimesafiri yapata wiki nne zilizopata. Utaratibu niliojiwekea ni kuhakikisha nafanya usafi wa nguvu katika nyumba yangu kabla sijafiri, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hakuna uchafu wa aina yoyote ile unaobaki ndani, mfano takataka katika dust bin, kuosha vyombo vichafu, usafi wa maliwatoni n.k.
Sasa leo asubuhi baada ya kurudi kutoka safarini nimekutana na mende mkubwa alikonda mpaka kufikia hatua ya kuwa mweusi katika korido, kitu ambacho sijawahi kukutana nacho maishani mwangu.
Mende huko ambaye baada ya dakika kadhaa alianza kurusha miguu kwa taabu sana huku akiwa chali na baada ya dakika mbili hivi alitulia tuli.
Kwa mara ya kwanza nimeshuhudia kifo cha mende live. Sikuwa na cha kufanya zaidi ya kumhurumia mende huyo.