Nimesikia hoja za Wizara ya Ardhi kuhusu kisiwa cha LUPITA

Nimesikia hoja za Wizara ya Ardhi kuhusu kisiwa cha LUPITA

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
525
Reaction score
2,950
Kwa tafsiri hii sasa ni wazi huyo @timdraper Tim Draper anayedai kuuza kisiwa chake LUPITA anajichekesha . Hata kama yeye ndiye alitoa fedha kujenga na kuwekeza huko LUPITA ,ila alitumia Kampuni ya Rafiki yake Tom Lithgow @lithgowtom kuwekeza inaiyoitwa Firelight Safaris Limited ya huko Arusha na ndiyo maana walimuingiza Tim Draper kwenye kampuni kwa kumpa hisa ya 25% ,huku mke wa Tom Lithgow Naitwa @belindalithgow akiwa na 24% ya hisa huku Tom Lithgow akiwa na 51% ya hisa.

Hivyo ,kwa namna hii ni kampuni ndiyo inayotambulika kuwekeza huko LUPITA na ndiyo iliyopewa Derivative rights na investment incentive. Hivyo ,haikuwa sahihi Tim Draper kutangaza kwamba anauza kisiwa ,hana hicho kisiwa wala hata uwekezaji inayotambulika ni kampuni tuu.Yeye ana hisa tuu kama shareholder na hatujui kama hiyo 25% ni thamani ya uwekezaji wake kwenye Kisiwa au laa ! . Hivyo yeye alipaswa ku-deal na kampuni ya Firelight Safaris Limited na sio kutangaza kwamba anauza KISIWA.

Hivyo,kwakuwa aliwekeza fedha zake kwenye Kisiwa hiki, inatakiwa aidha auze hisa zake hizo 25% , au kampuni iuze haki zake za uwekezaji (Derivative rights) kwa muwekezaji mwingine kwa njia ya ku-transfer ,sababu Derivative rights ni transferable alafu ndio achukue fedha yake baada mauzo hayo,ambapo anaweza kuamua fedha hizo baada ya mauzo zibaki kwenye kampuni hiyo katika uwekezaji mwingine wa kampuni hiyo sababu hiyo kampuni inaonekana kuwa na uwekezaji maeneo mengi na ni ya muda mrefu ili aendelee kupata dividend au achukue fedha zake asepe.

Pia Wizara Ardhi maelezo yenu ,mmeamua kufunika kombe tuu ,sababu hamjatueleza utaratibu uliotumika hadi kisiwa hicho kupatikana. Walikipataje?. Au ndio tusifukue Makaburi🤣🤣.Maana maelezo ya alikipataje ndio itasaidia kujibu hizo kauli zake Tim Draper ya kusema alinunua kisiwa mara aliuza Kisiwa. Tuambiwe alikipataje ,tusifunike kombe .

Soma Pia:
Ila tatueni changamoto za uratibu na mawasiliano kati ya Wizara ya Ardhi ,Wizara ya Utalii ,Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na TISEZA. Ni muhimu muunganishwe kwa taarifa na uratibu ili iwe rahisi katika majukumu yenu .Sababu taarifa zinasema Mwaka 2005 TIC wakati huo ilitoa certificate of incentive kwa kampuni ya Firelight Safaris Limited wakati kampuni haikuwa na kibali kutoka Wizara ya Ardhi kuwekeza kwenye Kisiwa kama (Public Land ).

IMG-20260831-WA0034(1).jpg
 
Back
Top Bottom