Nimesikia kuwa biashara ya kuendesha mchezo wa pool table inalipa sana

Nimesikia kuwa biashara ya kuendesha mchezo wa pool table inalipa sana

Hii biashara nilishawahi kuifanya,inalipa kweli,ila kama zilivyo biashara nyingine ina changamoto zake.Inahitaji mara zote kama mmiliki uwepo pale kwani mara nyingi wachezaji kwa kutokuwa waaminifu huwa wanachezea ule mtego unaofyatua mipira kwahiyo mipira iliyoingia ndani inaweza kutolewa bila ya kuingiza coin ya mchezo,hili linaweza kufanywa na wachezaji au msimamizi utakayempa hiyo kazi.Pool table moja miaka ile ilishafika mil.1 sijui kwa sasa bei zikoje,ziko za aina mbili kuna ambazo ubao wake wa kuchezea pale juu ni aina flani ya plywood huwa baada ya muda inapinda,meza za hivi zilikuwa bei ya chini kidogo,na nyingine zina aina flani kitu kama chupa inaitwa slate hizi zina bei ya juu kidogo zenyewe hazipindi.Inahitajika maintanance hasa ile mashine kila baada ya muda flani,kuna fimbo zile huwa zinavunjika,kuna kikofia juu ya fimbo huwa kinaisha ni lazima kila baada ya muda ubadilishe na kitambaa kile cha kwenye meza huwa kinachoka kinahitaji kubadilishwa....

Asante sana mkuu kwa mchango wako mzuri
 
Back
Top Bottom