Nimesikitika kuona wasanii wamegoma kwenda kumzika mama wa msanii mwenzao Chidi Benzi

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
25,968
Reaction score
36,044
Wasanii kwa wasanii wanaishi maisha ya kisanii ,maisha ya kinafiki , wanajifanya wanapendana kumbe upendo wa kinafiki.

Wasanii hupenda kuhudhuria shughuli iwe ni msiba, birthday,harusi nk ya mtu mwenye pesa , asiye na pesa wanamkalia mbali hata kama ni msanii mwenzao.

Kwa haraka haraka nakutajia mfano msiba wa mama Meja Kunta ulitokea mwaka jana, ila wasanii waliokwenda kumfariji hawakuzidi hata 10.

Msiba wa mama wa H Baba hivyo hivyo wamemlia buyu.

Juzi hapa amefiwa Chidi Benzi na mama yake naye pia wamemlia buyu haswa wasanii hawa wapya , waliohudhuria ni wale wasanii wa zamani sana .

Si waigizaji ,si wachekeshaji wala wana muziki wapya wamekwenda kumfariji mwenzao.

Ila sasa kama angekuwa Bi Sandra katangaza birthday ya Latifa ungeona hapo Lundo la wasanii kama nyuki. Ila kwa kuwa hao wengine wamechacha ,ndio maana wameliwa buyu na wenzao.

Hii inatoa picha halisi kwamba hawa jamaa sio watu hata kidogo, wapo kimaslahi muda wote.

Hapa kati Kikwete katoka kufiwa na shemeji yake, yani dada yake na Salma Kikwete lakini wasanii walijazana tele kwa kuwa wanajua wataokota chochote kitu.
 
Tafuteni pesa muache kulalamika
Kilichotokea hapo umekiona kwa sababu ni msanii ila mtaani kwa kila mtu hapa msiba wa maskini watu kumi wa tajiri watu mia
Acheni kuwalaumu wasanii kama hamuyaoni haya yanayotokea kwenye mitaa yenu kila siku na hao wasanii ndio ndugu zetu tunaishi nao
Tofauti ipo kwenye means ya utafutaji tu
 
Kwahiyo we maisha yako umewekeza kufatilia nani hahudhurii misiba ya watu? Huna kazi ya kufanya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…