Nimesikitishwa na Habari ya Watanzania Kupendelea Parachichi za Burundi Kuliko za Tanzania. Watafiti Wetu Mnafeli Wapi?

Hapo kwenye embe kuna siku nilikuwa dar nikanunua embe dodo buku chachu hatari kama bongwa nikaenda kijijini nikanunua dodo hilo hilo mia 3 embe tamu kama asali dodo kubwa hatari na nina mpango ule muembe niufanyie grafting nipande mazao ya kudumu

Mimi niliyekulia kijijini najua huo mchezo hayo maembe huwa wanachuma mabíchi halafu wanayapepea kwenye moto ukibonyeza yameiva ukila machachu hatari

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Yaani parachichi za Burundi kuubwaa, very soft na zina mafuta na ladha muruaa, hata wakiuza elf 5, watu watanunua!! Sasa haya ya kwetu, kwanza hazikomai, ndani majimaji na kambakamba tuupu!! SUA mna jambo la kufanya mtusaidie!!
unakuta mtu hajasomea kilimo naye anazalisha miche pumbavu sana

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Embe Bongwa sasa hivi zimeadimika, aisee ile embe ni chachu sijawah kuona
 
Janja janja ndio shida kubwa ya Mtanzania
Wanachuma Parachichi kabla ata azijakomaa na kuzivundika - zinafika sokoni azijaiva ipasavyo na azina ladha, na zingine zina fungus. Ukila kama unakula makapi no taste
 
Unanunua parachichi ndani jeusi minyuzi nyuzi kokwa kubwa kuliko nyama sometimes nyama ngumu,havina mafuta vimejaa maji.

Kimsingi bongo tunafeli sana kwenye ubora.

Za burudi ni makubwa,malaini matamu,mafuta mengi yana vutia,hata ungekua wewe mleta mada ungechagua yepi?
 

..parachichi zinazopendwa ktk nchi za ulaya na marekani ni zile ndogo zinazolimwa Tanzania.

..parachichi kubwa-kubwa kama za Burundi haziuziki ktk mataifa hayo.

..tunachotakiwa kufanya Watanzania ni kuhakikisha parachichi zetu zinakuwa ktk ubora wa kimataifa.

..pia tunaweza kulima parachichi za Burundi na kula majumbani kwetu, na parachichi za Kitanzania tukauza nje.
 


Sio tatizo kabisa, tena napongeza hiyo tabia.
 
Unazungumzia Maparachichi ya kuuziana mtaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…