Nimesikitishwa na Habari ya Watanzania Kupendelea Parachichi za Burundi Kuliko za Tanzania. Watafiti Wetu Mnafeli Wapi?

Nimesikitishwa na Habari ya Watanzania Kupendelea Parachichi za Burundi Kuliko za Tanzania. Watafiti Wetu Mnafeli Wapi?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Chonde chonde Wataalamu wa utafiti wa Parachichi fanyeni hima mkajifunze Burundi au fanyieni utafiti Parachichi za huko ni Kwa nini zina Radha nzuri,laini na kutoa juice zaidi kuliko za Tanzania.

Vinginevyo Tunaenda kuua soko la Parachichi zetu kama msipofanya jambo.

=====
Mahitaji ya parachichi kutoka Burundi yanaongezeka licha ya bei yao kubwa kwani watumiaji wanapendelea parachichi hizo kuliko zile zinazozalishwa ndani kutokana na ukubwa, ladha, na laini yake.

Uchunguzi wa 'Daily News' katika maeneo ya Buguruni na Mabibo, vituo vikubwa vya jumla na rejareja vya kuuza parachichi, ulionyesha bei ya parachichi za kutoka Burundi ni mara tatu hadi nne zaidi ya bei za zile za ndani - kwa kawaida kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Iringa, Njombe na Mbeya.

Uchunguzi ulifunua kuwa bei ya parachichi za Burundi inatofautiana kati ya 1,500/- na 1,700/- ikilinganishwa na kati ya 300/- na 1,000/- za ndani.

Muuzaji wa parachichi kwa jumla na rejareja huko Buguruni, Bwana Mohamed Temi, alisema siku ya Jumapili kuwa licha ya kuwa msimu wa parachichi, mahitaji ya parachichi za Burundi bado yalikuwa juu na hivyo ndivyo bei yake.

“Watu wanapendelea parachichi hizi licha ya bei yao kubwa kutokana na ladha nzuri, muundo wake, na laini yake," Bwana Temi alisema, "pia, parachichi hizo zinautoa zaidi wa maji ukilinganisha na za ndani." Aliongeza kuwa bei zake za jumla na rejareja zinaenda vizuri kwani hana upungufu wa wateja.
 
Kwetu kila kitu kiko out of control, japo zipo board kibao zinafanya semina, vikao, training na mishahara minono, lakini huko kwenye ground hakuna kinachoendelea.
Tuna mdomo sana ila akili ndio hizo za kina Mruma cc bandari
 
Itatu cost na kuua Kilimo Cha parachichi,mara wavune mazao ambayo hayajakomaa nk hii sio sawa
Kama embe za Tabora. Wana embe nzuri sana lakini njaa njaa zao na tamaa huwa wanazivuna zikiwa changa halafu zikianza kuchoka na kulegea wanasema ndiyo kuiva. Ukiwauliza kwanini mmachuma changa, bila ya aibu wanajibu wanawahisha sokoni, wengine wanasema ndiyo zinachelewa kuiva...mazakanywa fanta zao
 
Kama embe za Tabora. Wana embe nzuri sana lakini njaa njaa zao na tamaa huwa wanazivuna zikiwa changa halafu zikianza kuchoka na kulegea wanasema ndiyo ku8va. Ukiwauliza kwanini mmachuma changa, bila ya aibu wanajibu wanawahisha sokoni, wengine wanasema ndiyo zinachelewa kuiva...mazakanywa fanta zao
Duu njaa ya umaskini mbaya sana
 
Parachichi za Burundi zina unga mtamu za TANZANIA zina maji mengi kutokana na utunzaji mbovu
Yaani parachichi za Burundi kuubwaa, very soft na zina mafuta na ladha muruaa, hata wakiuza elf 5, watu watanunua!! Sasa haya ya kwetu, kwanza hazikomai, ndani majimaji na kambakamba tuupu!! SUA mna jambo la kufanya mtusaidie!!
 
FB_IMG_1628091025771.jpg
 
Back
Top Bottom