Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 143,138
- 288,731
Ni wapi aliomba msamaha?Atasamehewa baadaye
Aende ACT kufanya nini? Hakuna anayeweza kupata ubunge kwa Tume feki ya KailimaLkn anakwenda ACT...
Wale wenzake je, wametimuliwa?
Makosa yake haya samehekiAtasamehewa baadaye
HayaUnatuletea upuuzi eti hauziki!Sasa nyie mliokuwa mnajaribu "kumuuza" tuwaiteje?
Wapuuzi,wajinga au wendawazimu?Mrema alikuwa kiongozi wako leo unadiriki kumponda?Sio ajabu kwani hata Mbowe uliyekuwa ukimuita mwamba leo unamponda!Wewe ni ndumilakuwili usiyekuwa na msimamo na hustahili hata kufunga kamba za viatu za Mrema.Mremq ameonyesha guts za kupigania anachokiamini sio sawa na wewe bendera kufuata upepo.
Ni kweli, Mrema anachukuliwa poa tu tofauti na MsigwaKitendo cha John Mrema kufukuzwa Chadema ni cha kusikitisha mno, hasa ikizingatiwa kwamba, Mtu huyu tumeshirikiana naye katika mengi ndani ya Chama, (ofisi ya Katibu Mkuu imethibitisha kupokea barua ya kutimuliwa kwake kutoka tawi la Bonyokwa), Hakika laana ya Usaliti inatisha.
John Mrema alikuwa kiongozi wa ngazi ya Juu ya Chadema, akihudumu kama Mkuu wa Itifaki, huyu alijua ajenda zote za Chama chake, ndiye aliyekuwa ripota wa mambo yote ya Chadema kwa Waandishi wa Habari, aliripoti aliyoshiriki kuyaamua, Kitendo cha yeye kupinga ajenda ya Chama chake, iliyotolewa akiwa Madarakani bila shaka yoyote ni Usaliti.
Lakini Je kwanini Mrema alisaliti msimamo wa chama chake wa Ajenda muhimu aliyoshiriki kuitengeneza, Je alinunuliwa? Swali hili ndilo analouliza kila mtu.
Je huyo aliyemnunua (kama ni kweli) alimfahamu vizuri Mrema?
John Mrema pamoja na kuhudumu kama kiongozi wa Juu wa Chadema hakuwahi kuwa na ushawishi wowote ule nje ya Madaraka aliyopewa, si mtu ambaye angeweza kushawishi yeyote kwenye majukwaa ya hadharani, hakuwahi kuwa na Ushawishi huo, hili hata yeye anajua, 2020 aliangushwa kwenye kura za maoni za kuwania Ubunge wa Jimbo la Segerea, busara ikatumika ili kumpitisha, kwa muda wote Mrema alisafiria nyota ya CHADEMA tu, Japo nakiri kwamba alifanya kazi vizuri sana, Kazi aliyofanya John Mrema haikuwa rahisi kuitoa dosari, Lakini alikosa karama ya ushawishi, Jambo ambalo kwa Mwanasiasa ni kosa kubwa. Si kazi rahisi kumnadi Mrema Jukwaani, Hauziki.
Ninamtakia kila la Heri huko aendako.
Ana hoja gani? ziweke hapa nijibu mimi sasa hiviUsiache mbachao kwa msala upitao. Hivi mnadhani kumuita msaliti ndio kutajibu hoja zake?
Mrema alikuwa ndio sura ya Chadema na anajua analofanya. Kama mwanachama wenu yeyote aliye fukuzwa na tawi anakuwa hana haki ya rufaa basi matatizo ni makubwa.
Jibuni hoja zake badala ya kuonyesha kuwa hamna tofauti na CCM.
Amandla...
Wako 55 tu, Chadema ina wanachama mil15Criticism kwa sasa ni mwiko ndani ya Chadema.
Atachoamua Lissu ni kama msahafu au bible, ni mwiko kukosoa.
Udikteta ndani ya Chadema hauwezi kuleta mwisho mzuri.
Swali ni je mtafukuza wangapi?
Hoja zijibiwe kwa hoja.
Mkutano wa Januari 2020 wa Chadema huko Makueni Kenya uliaamua nini?Maazimio gani yalifikiwa?Ana hoja gani? ziweke hapa nijibu mimi sasa hivi
Una muamini?Ziko kwenye uzi huu.
John Mrema: Hakuna kikao kilichopitisha suala la kuzuia uchaguzi
Amandla...