Nimesimamishwa kazi kwa kosa la kutokufika kazini, je nifanyeje?

Nimesimamishwa kazi kwa kosa la kutokufika kazini, je nifanyeje?

ainisha kwenye barua aliyokuandikia - kutofika kazini ndiyo uchunguzi?
kasome sheria za kazi - ni lini mfanyakazi atafukuzwa kwa kosa la kutofika kazini , kuna due process lazima zikamilike akibana sana mwambie mtaonana mahakama ya kazi- ni pm nitakupa number a good lawyer - NO WIN NO FEE.
Naomba msaada wa kisheria kuhusu uhamisho wa mke wangu maana nimekuwa nazungushwa sana
 
Hao dawa yao ni ndogo sana,wewe tulia hadi wakufukuze kazi halafu wapeleke wahakamani ukishashinda kesi then dai fidia........hawana akili wanacheza na haki za watu bila kujua catastrophic effects yake!!......kesi kama hiyo hata mtoto wa chekechea anashinda!!
Hakunaga fidia (gharama za kesi) kwny kesi za kazi. Yeye akienda mahakamani akadai KURUDISHWA KAZINI ama kama inashindika basi KUPEWA SITAHIKI YAKE ila sio eti afungue kesi akishinda (after judgment if wins...) adai fidia. Hiyo sio normal civil case hyo ni labor case...
 
Wakuu habari za mchana na poleni kwa majukumu.

Nimeajiriwa kama mwalimu katika shule moja inayomilikiwa na kanisa. Mnamo tarehe 07/04/2017 mkuu wa shule alitutaka tufike kazini japo ilikuwa ni sikukuu ya kitaifa (Karume day). Nilitoa udhuru kwamba licha ya kuwa ni siku ya mapumziko pia nilikuwa na masuala ya kifamilia niliyopanga kurekebisha siku hiyo.

Baada ya siku hiyo mkuu alikuja akatangaza kuwa anatoa likizo kwa wafanyakazi wote kuanzia tarehe 12/4-23/4/2017 isipokuwa mimi niendelee kufika kazini kama kawaida. Nilitimiza amri yake na kufika shuleni siku zote bila kunung'unika au kulalamika hadi jana shule ilipofunguliwa.

Cha ajabu ni kuwa leo amekuja na kunitaka nikabidhi mali za shule na kunipa barua ya kunisimamisha kazi afanye uchunguzi halafu ataniita kwa utetezi.

Kosa kwenye barua ni hilo la kutofika kazini siku hiyo.
Sina rekodi ya makosa na sijawahi kupewa barua yoyote ya onyo.
Kwa ninavyomjua ni dhahiri kuwa kifuatacho ni barua ya kunifukuza kazi.
Ninaomba ushauri wenu nifanye jambo gani maana naona wazi haki zangu zinaminywa na mkataba wangu unaelekea kumalizika.

Natanguliza shukrani zangu kwa ushauri mtakaonipatia.
Kama ww ni mwajiriwa wa umma soma na PUBLIC STANDING ORDERS 2009 kipengele cha kutofika kazini nini huwa cha kufanya....itakusaidia na siku nyingne.
 
MKUU KAMA UNA MKWANJA WA KUSOGEZA SIKU ZA KARIBUNI WE TULIA ALAFU WAKIKUFUKUZA KAZI TUNAENDA FUNGUA KESI NA TUNAPATA FIDIA TA BREACH OF CONTRACT
 
Wakuu habari za mchana na poleni kwa majukumu.

Nimeajiriwa kama mwalimu katika shule moja inayomilikiwa na kanisa. Mnamo tarehe 07/04/2017 mkuu wa shule alitutaka tufike kazini japo ilikuwa ni sikukuu ya kitaifa (Karume day). Nilitoa udhuru kwamba licha ya kuwa ni siku ya mapumziko pia nilikuwa na masuala ya kifamilia niliyopanga kurekebisha siku hiyo.

Baada ya siku hiyo mkuu alikuja akatangaza kuwa anatoa likizo kwa wafanyakazi wote kuanzia tarehe 12/4-23/4/2017 isipokuwa mimi niendelee kufika kazini kama kawaida. Nilitimiza amri yake na kufika shuleni siku zote bila kunung'unika au kulalamika hadi jana shule ilipofunguliwa.

Cha ajabu ni kuwa leo amekuja na kunitaka nikabidhi mali za shule na kunipa barua ya kunisimamisha kazi afanye uchunguzi halafu ataniita kwa utetezi.

Kosa kwenye barua ni hilo la kutofika kazini siku hiyo.
Sina rekodi ya makosa na sijawahi kupewa barua yoyote ya onyo.
Kwa ninavyomjua ni dhahiri kuwa kifuatacho ni barua ya kunifukuza kazi.
Ninaomba ushauri wenu nifanye jambo gani maana naona wazi haki zangu zinaminywa na mkataba wangu unaelekea kumalizika.

Natanguliza shukrani zangu kwa ushauri mtakaonipatia.
Ok
 
Hakuna sheria inayoradhimisha mtu kwenda kazini siku za weekend au sikukuu cha kwanza onana na chama cha kutetea watumishi mfano cwt
 
Hakuna sheria inayoradhimisha mtu kwenda kazini siku za weekend au sikukuu cha kwanza onana na chama cha kutetea watumishi mfano cwt
Hakuna kitu kinaitwa weekend kwenye sheria za kazi.
1.kuna siku sita za kazi kwa wiki.....wiki itaanza kuhesabika pale ulipo anza kazi kwa mfano kama ulianza kazi siku ya Jtano utaanza kuhesabia siku ya kwanza ya wiki siku hiyo, kabla ya kuanza kazi siku nyingine utatakiwa kupumzika masaa 12 na kabla ya kuanza wiki nyingine unapaswa kupumzika masaa 24.
2. Kufanya kazi Jtatu -Ijumaa au Jmosi ni mazoea tu; na hasa yamejengeka ktk misingi ya imani za kidini

Note: Sheria inatambua siku za sikuu za kitaifa kuwa ni siku za mapumziko na kama utafanya kazi siku hizo unastahili ujira mara mbili.(Rejea ELRA NO:6/2004 Sect. 17-23.
 
Siku za masomo kwa taasisi za elimu ni siku 194 kwa mwaka hapo siku za weekend hazijajumlishwa kwa mwaka huu 2017.
 
Sasa kipi sahihi mnatunchanganya sasa tuelewe lipi hapo ?
Yeah, ELRA NO.6/2004 chini ya G.N.47/2017 sasa inatambua kitu kinacho itwa Breach of contract. Ktk breach of contract unafidiwa kile kipindi cha mkataba kilicho baki. Pia kwenye unfair termination ipo remedy ya compensation chini ya kifungu cha 40(1)C cha ELRA. ambayo si chini ya mishahara ya miezi 12 ama kiwango kingine kwa kadri uzito wa shauri utakavyo kuwa.
 
Back
Top Bottom