hapana, hapana, DARUSO ilijitahidi kadiri ilivyoweza ila utawala ndio ukawa kikwazo!
Kumbuka ili resolutions za USRC ziwe halali ni lazima zifanyike katika kikao rasmi. Katika semista hii, USRC ilipangiwa kikao kimoja tu, ambacho ni cha tar. 7 Januari. Jitihada za ofisi ya Spika kupata kikao cha dharura siku ya tar. 11 Novemba mwaka jana, na kile kipindi cha kufukuzwa kwa wenzetu 41, zilikwamishwa kwa makusudi na utawala wa chuo. Sasa huko kukosa umoja kunatoka wapi ndugu?
Na kama ingekuwa hatuna umoja na wenzetu, kwenye kikao cha juzi tusingepitisha mgomo kwa ajili ya 41 waliofukuzwa. Tuna hisia pia, wale ni wenzetu, jamaa zetu, rafiki zetu, mademu zetu na mabwana zetu pia. How can we be so feelingless towards our beloved ones?