Pole sana ila kwanini umeogopa kuja na ID Yako ya zamani? Unanipa mashaka kama kweli wewe ni mpigania haki au bendera.
Mnapokuwa Viongozi feedback ni muhimu sana kwa wale mnaowaongoza ni nani Mwana UD alijua kuwa mlikuwa mnakosa VENUE? kama mliamua kukaa kimya hamkuona si utawala Bora huo ? Kiongozi panapotokea hali yoyote ile ya matatizo au mazuri cha kwanza ni Taarifa? Leo hii hakuna Mwana UD utakaye Mwambia mlikuwa bega kwa Bega ili kushughulikia matatizo yote yale yaliyokuwa yakitokea. Ni wazi kuwa mliweka matabaka kiasi cha kulaumiwa na Wanachuo wote hadi wanachuo wakataka kuanza harakati za kuuondoa Uongozi wa chuo madarakani? Je Mlikuwa wapi toka harakati zinaanza Mbona zilitolewa makala kibao za kushindikiza wanafunzi waache migomo kwani wanavunja sheria.Mliona nini kutoa makala kama hizo na za kueleza umma kuwa Utawala unaweka vikwazo kama hivyo? Leo hii hakuna anaeona uchungu kwa kuondoka kwenu kwani kila aliyekuwa akidai haki aliwachukulia kama wasaliti tu.....Leo hii kimya chenu cha muda mrefu ndio kimezua balaa lakini kama kiongozi taarifa ni Muhimu sana ...mwanaphilosophy Jean Jacques Rousseau alisema
''Absolute silence leads to sadness. It is the image of death''.
Si vibaya kuja na ID mpya ila hata mimi nashaka kwanini kwenye haki yako uwe Muoga? hapa ndio panaponitia wasiwasi kwani uliyoyafanya wewe ni kuua mtu au? Mi nadhani kama vyombo vya hbr vinatoa hbr hizi wewe uliyeathirika unajificha nani atakusaidia? Je leo Wakija TBC kwa kutaka uwaeleze nini kilitokea utaficha sura yako?
hapana mkuu. Haya ni masuala ya jamvini, hata ningekuja na ID yangu ya siku zote, ni wachache sana wanaonifahamu in personal humu. Na karibu wote wanafahamu chenye kilinikuta...
Naomba nieleweke ivo untill further notice.
Uhuru una gharama kubwa, hongera kwa ajili ya uhuru, pia pole kwa ajili ya mwili. kama hutojali waweza nijibu, wewe ni mtz, mkenya au mbaganda.
Sasa kusimamishwa masomo wana udsm na Chadema vina uhusiano gani?? Mbona hujasema CCM itamlipia masomo india?? I dought you might be having a.al fistula.
Wanafunzi wengine waliotimuliwa ni pamoja na Mkenda Paul, Msigwa Pangani, Nafti Daniel, Mwasakafyuka Edward,
Amoni Stephano, Wilfred Bocasa, Garubindi Gaston, Mwalusanya Wilfred, Mwalo Innocent na Malipula Edgar.
Pole sana Mkuu, usiwe na wasiwasi Chadema watakupeleka India ukasome ndio upambanaji hakuna haja ya kulia lia
well said mkuu.
Jamaa ni watu wa visasi sana, hawachelewi kukomoa kabisa, kuzungumza nao kuna-make sense kwa sasa kuliko kukimbilia mahakamani, ukizingatia jamaa wana back-up ya mkuu wa kaya.
haki ya mtu haipotei na daima tutashinda hii vita ya ukandamizaji mnachokipigania kimanufaa kwa wengi kwame siwalaumu nasintothubutu ..maamuzi ya daruso ni halali kabisa kwani ndio chombo halali cha kuwawakilisha wanafunzi hapo udsm .. Migomo imesadia wengi nikiwamo mimi .. Kuna watu wengi wamesumbuliwa sana kwa kutetea umma wa wanaudsm na vitisho vingi ila mwisho wa siku tuko nao na mtaani wanaendeleza pambano mfano mzuri ni david silinde(mbunge mbozi magharibi ) mpaka mahakama walimpeleka mtatiro julius (naibu katibu mkuu cuf bara) na wengine wengi tu so kamanda usiogope utashinda kwani mtachotetea ni haki yenume sikupi pole, ila nakutia moyo. Me niko home toka mwezi wa 6 last year baada ya mgomo, nimehojiwa nasubiria majibu yao. Ila bilieve me hali hii imenijenga nakujua maisha hasa. Utakutana na wengi watakaokulaumu hata wa2 wa karibu, usiwamind we waeleweshe au wapotezee pia wapo wachache watakao kutia moyo. Ts just a mater of time..haki ya mtu haipotei
well said mkuu.
Jamaa ni watu wa visasi sana, hawachelewi kukomoa kabisa, kuzungumza nao kuna-make sense kwa sasa kuliko kukimbilia mahakamani, ukizingatia jamaa wana back-up ya mkuu wa kaya.
Kwema wanajamvi?
Kama kichwa kinavyojieleza, nilipokea ujumbe kutoka ofisi ya Mshauri wa Wanafunzi saa 3 hivi asubuhi, ikinitaarifu kuwa nisubiri chumbani kwangu niletewe barua yangu. Karibu saa 7 hivi, baada ya kusubiri sana uvumilivu ukaniisha, nikaenda Nyerere Campus, nikapata barua yangu pale Auxilliary Police, iliyoeleza, nanukuu, "RE: SUSPENSION FROM STUDIES PENDING INVESTIGATION
Be informed that following your participation in the making of an illegal USRC desicion to defy Council orders, you have been suspended from studies pending futher investigation...", mwisho wa kunukuu. Nikakabidhi kitambulisho cha chuo kwa askari, tukaonana na viongozi wenzangu wa DARUSO, tukafarijiana na kuelekezana cha kufanya wakati huu mgumu.
Saa 11 jioni nikawa Mabibo Hostel kufanya taratibu zote za kuondoka chuoni, saa 11:30 hivi nikaondoka maeneo ya hostel kurudi nyumbani, ninakoishi.
Hii ni ID mpya, anayehitaji taarifa zaidi ani-PM.