Nimesitisha wazo la kuuza nyumba yangu

Nimesitisha wazo la kuuza nyumba yangu

Dalali wa mjini

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2024
Posts
326
Reaction score
464
Habari ndugu zangu.

Nilileta uzi WA kutaka ushauri WA kuuza nyumba yangu, baada ya kupitia comments Za nyinyi wanandugu nimeona comments nyingi zikisema nisiuze nyumba yangu.

Ushauri wenu nimeupokea Kwa mikono miwili Na Kwa Moyo mkunjufu Na Kwa akili zangu timamu.Jana nimeshauriana Na Mke wangu usiku mrefu baada ya kukosa usingizi ikanibidi nimuamshe ili tuongee juu la swala hili la kuuza nyumba lakini ukweli mke wangu alikataa huku akitaka kulia lakini badae akakubali kishingo upande.

Katikati ya Mada nikamwambia tukate kiwanja pale nyumbani tukiuze ibaki nyumbani Tu kwajili ya wapangaji mana nyumba tumeipangisha.Wazo likapita Na tumekubaliana tuuze kiwanja na pesa inayopatikana tununue Gari nifanye Uber mana Mimi Ni dereva pia ili kukidhi mahitaji muhimu Na Kodi Za hapa mjini.

Kwahiyo ndugu zangu nawashukuru Sana Kwa ushauri wenu,Hakika hili jukwaa Ni shule kabisa.Sasa hivi kiwanja nakiuza kwajili ya Hilo Jambo la kununua Gari lakini biashara ya udalali siwezi acha itanifikisha Mbali.

Wale wanataka kwenda kutafuta Maisha South Africa nawashauri wasijaribu kabisa mana watalia wakifika kule labda kama wanaenda Kwa ndugu zao Na hata kama wataenda watenda kuona ukweli wa mambo.Souz imekuwa ya kifala sana hakuna kama Zamani yaani inaitwa aliepata kapata aliyekosa hawezi kupata Na inabidi arudi nyumbani mana mwisho wa siku unaweza kuishia kwenye uvutaji wa madawa kwajili ya mawazo kule south Africa.

Asante Sana JamiiForums
 
Back
Top Bottom