Nimestaajabu ushauri wa dakitari

The Infamous

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2009
Posts
731
Reaction score
121
Nimeweka kijiti cha kuzuia mimba, nikaambiwa ntakutana kimwili na mpenzi wangu baada ya 24 hrs. nikafuata ushauri huo. lakini baada ya mwezi na nusu nikagundua na mimba, ikabidi niende private hospital kupata ushauri, dakitari akasema hukutakiwa kukaa 24 hrs, bali ulitakiwa ukae 10 days, bila kukutana kimwili, kwa sababu nilikuwa sijajiaanda na ujio wa huyu mtoto ikabidi mimba itolewe.

Lakini nikamuuliza dakitari, vipi kuhusu hii njiti, nayo nikaitoe au lah, akasema haina shida yenyewe itaendelea kufanya kazi hivyo usiitoe, nikaiacha kwa kufuata ushauri huo, cha kushangaza baada ya mwezi toka nifanye dhambi ya utoaji, nimejigundua na mimba tena...nimestaajabu sana.

Nauliza madakitari, shida hasa ni nini hapa, njiti haina kazi, haikufanya kazi au ushauri niliopata haukuwa sahihi, maana mpaka sasa njiti bado ninayo na sijaitoa....
 
Acheni ngono zembe' ona sasa kwanza ushaua na huyu tena lazima umuue tena bila shaka!
 
huyu wa pili siwezi kamwe. mola anisamehe. life is so challenging.
 
Jamani ila na we unapenda kufanya mapenzi... pole vumilia hivyo vijiti havichomi chomi?
 
Huo mjiti rafiki ukikosea kuwekwa unapata ujauzito...bila shaka umekosea kuwekwa na ndio maana haufnyi kazi ipasavyo...cha kufanya ni kuutoa uwekwe mwengine au utumie njia nyingine za uzazi wa mpango!
 
kwa nini sasa ulitoa mimba umenisikitisha sana kuua kiumbe kisicho na hatia halafu wasema hadharani loh
 

My advice to you is COMMIT SUICIDE!!! WHY??? Because Life begin at conception. Ulipotoa mimba umefanya dhambi ya mauaji. Umedhulumu nafsi ya mtu. According to THE TIBETAN BOOK OF LIVING AND THE DEAD. Mwanamke akitoa ujauzito, nafasi ya mtoto ambaye ujauzito wake ulitolewa hurejea tena baadaye kupitia kikojoleo cha mwanamke huyo huyo. But safari hii mtoto huyo hurejean tena duniani kwa lengo la kulipa kisasi kwa muuaji wake. Na kisasi hiki hulipwa kwa kuchukua nafsi ya mtoa ujauzito. So kitakacho tokea utakufa ukiwa unatoa mimba nyingine au mtoto atakaye zaliwa atasababisha kifo chako hapo baadaye kwa namna moja au nyingine.

SOLUTION : ACHA UONYIBERIBE! GO AND CONFESS AND DO NOT DO SUCH A FETISH ACT AGAINOOOO!
 
Kinachonishangaza ninyi ndada zetu vichwa vipo resi sana sasa kwanini msitumie njia salama kama safe days na external ijaculation?ona umemuua mbunge sasa unahakika gani kua ulowaacha huko tumboni ni majambazi?iko siku mtaambiwa muweke hata magogo sio njiti.duh. be areful
 
Nakupa ushauri :Ukienda kuweka kijiti unatakiwa kuwa kwenye siku zako , sasa kama ukienda tofauti na hapo ndo mimba yenyewe pia katika hili hospital za serikali ni wazuri sana, sasa cha pili ni kazi ya daktari kukuwekea kijiti ambacho hakija isha muda wake,tatu ondoa kijiti acha hormone zikae vizuri na kama unampango wa kuzaa muandalie pre-natal wako mazingira mazuri.
 
Mzae uniletee mimi nitamlea. Kama unataka details zangu just contact me.

Nangu mahwelu.
 
imebidi niwe muwazi ili mchangiaji aelewe tatizo kiundani wake, hatahivyo sihalalishi hii dhambi, itabaki kuwa dhambi. pole kwa kukukwaza.
 

Kabla madakitari hawajakujibu....................... andaa majibu utakayotoa siku ya kiama kwa dhambi ya mauaji!
 
Unaweza kutumia pia sindano za mzazi wa mpango ila usiamini sana kama unaweza bora utumie period zako au kondom hizi njia nyengine ni plus au minus kila siku utaingia kwa majanga usipoangalia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…