Nimestushwa sana kusikia mtangazaji Wasafi Media, anayeitwa Adela, akijimwambafai kuwa amewahi kuhongwa milioni 60 na mpenzi wake!

Nimestushwa sana kusikia mtangazaji Wasafi Media, anayeitwa Adela, akijimwambafai kuwa amewahi kuhongwa milioni 60 na mpenzi wake!

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Nafuatitilia kipindi Cha Wasafi Media, kinachorudhwa LIVE muda huu, ambacho kimepewa jina la HAUJUI, nikishuhudia mtangazaji wa Wasafi Media, Oscar Oscar, akimuuliza mtangazaji mwenzake anayeitwa Adela, akimuuliza awe mkweli na amwambie katika maisha yake , anakumbuka ni kiasi Gani alichowahi kuhongwa kikubwa na anakumbuka ni kiasi Gani??

Msichana huyo bila aibu Wala kusita amejibu kuwa aliwahi hongwa na Bwana tu aliyekuwa akitembea naye shilingi milioni 60 Kwa mpigo!

Nimestushwa sana na huo ushuhuda aliotoa huyo mdada, ingawa hakumtaja huyo mtu wake "kibopa bilionea" lakini Mimi naamini kuwa atakuwa mwanasiasa, kutoka Sisiem!

Kwa kuwa pia naamini kuwa huyo "kipopa bilionea" atakuwa amefanya wizi wa Kula Kwa urefu wa kamba yake!

Kwa kuwa Rais Samia alishawapa "green light" hao wateule wake, wale Kwa urefu wa kamba zao, Kwa kuwa siamini kama atakuwepo mfanyibiashara yoyote atakayekuwa na "wehu" huo wa kuhonga pesa nyingi kiasi hicho, tena akiwa ni kimada tuuu!

Kwa kuwa najua Kwa mfanyibiashara yeyote wa nchi hii hata akiwa "level" za akina Bakheresa, hawezi kufanya uendawazimu wa aina hiyo, ukizingatia mlolongo wa makodi ya TRA yanayomwandama Kila kona
 
Nafuatitilia kipindi Cha Wasafi Media, kinachorudhwa LIVE muda huu, ambacho kimepewa jina la HAUJUI, nikishudia mtangazaji wa Wasafi Media, Oscar Oscar...
Mpenzi hahongwi, huyo ni malata tu
 
Wewe hata muda wa kuwasikiliza/kuwatazama unao??
Hahahahaha..... 😅

Sasa kosa langu ni lipi hapo??

Je kumtizama huyo dada akijimwambafai, kuwa amewahi kuhongwa na mpenzi wake shilingi milioni 60 Kwa mpigo, imekuwa kosa??😁
 
Hahahahaha..... 😅

Sasa kosa langu ni lipi hapo??

Je kumtizama huyo dada akijimwambafai, kuwa amewahi kuhongwa na mpenzi wake shilingi milioni 60 Kwa mpigo, imekuwa kosa??😁
Maana yangu ni kwamba hawana kitu cha msingi cha kumfanya mtu mwenye akili timamu awasikilize.
 
Nafuatitilia kipindi Cha Wasafi Media, kinachorudhwa LIVE muda huu, ambacho kimepewa jina la HAUJUI, nikishuhudia mtangazaji wa Wasafi Media, Oscar Oscar...
Takukuru walikuwa na pa kuanzia kumnasa m CCM bazazi huyo
 
Nafuatitilia kipindi Cha Wasafi Media, kinachorudhwa LIVE muda huu, ambacho kimepewa jina la HAUJUI, nikishuhudia mtangazaji wa Wasafi Media...
Pengine ungeweka sura/picha ya huyo Adela tuone kama anastahili kuhongwa hata 50,000? Kwenye msiba Fulani huko kwao ilikua aibu. Ashukuru kamati ya mapambo walificha-ficha mbavu za mbwa huko migombani kwao. I'm sorry
 
Mchaga wa watu kaona hapati promo kaamu aje Kwa staili yake na kujipandisha thaman Ili mafisi yakamchungulie ana nn mpk aongwee m 60 ...

Ila n karembo semaa m 60 ni nyingiiiiii
 
Back
Top Bottom