Nimesugua sana benchi, je postgraduate diploma ya education out yaweza kuwa msaada kwangu..?

Nimesugua sana benchi, je postgraduate diploma ya education out yaweza kuwa msaada kwangu..?

NG'HOMELE

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2014
Posts
470
Reaction score
147
Wana jf, mimi nimehitimu degree ya project planning, management & comunity development mwaka 2011 lakn mpaka leo sijafanikiwa kupata ajira ama serikalini au kwenye mashirika binafsi zaidi nimejiajili mwenyewe na shughuli zangu binafsi lakn nataman sana siku moja nipate ajira serikalini kwani kuna security. Naomba msada wenu wa kimawazo kwani nataka mwaka huu nikasome PGDE ya open university of Tanzania, swali langu ni kwamba, pindi nimalizapo masomo yangu naweza pata ajira ya moja kwa moja kama wale wenye degree, diploma, na certificate? Pili, je hawa OUT hawana ubabaishaji mana nasikia kuna watu wanasomea kazi za watu kwa kubadilisha jina kwenye centre husika pindi zipokewapo toka posta? tatu, je muda wa masomo ni mwaka mmoja au miwili? je huwa kuna field practical? nne, je ni kweli kuwa gharama zao ni zaidi ya mil. 2.5? tano viwango vya mshahara vya mshahara na wale wenye degree iko sawa na wale wenye PGDE? Ahsanteni na Mungu awabariki
 
Check kwenye tovuti yao mambo ya malipo na muda wa kusoma hiyo kozi husika. Je unataka kusoma hiyo postgraduate ili uajiliwe na serikali kama mwalimu??? kwa namna trend ya mambo yanavyokwenda soko la waalimu wa arts litakuwa limejaa siku si nyingi sana. Kama utaajiliwa mwaka huu kwa sifa linganishi sawa, lakini kama hujaajiliwa....fanya mambo yako ya maana zaidi.....haya ni mawazo tu sio kanuni.....I stand to be corrected.
 
Nashukuru kwa ushauri wenu, na masomo ya sayansi lkn
 
Komaa tu utatoka maana walimu wanahitajika. Kasome tu au nenda udom mwaka huu mwezi wa kumi unaweza pata nafasi
 
Ndio ni udom kwani ud nao wana hyo koz
 
Postgraduate Diploma in Education(PGDE)
UDOM -wanayo hiyo program.
UDSM- Wanayo hiyo program,ila ni Regular(vipindi muda wowote kwa siku e.g asubuhi,mchana,jioni)
UDSM/DUCE CAMPUS- Pia wanayo hiyo program,ilianza February 2013, ni EVENING PROGRAM.
 
Shukran sana wadau lakn mi shida yangu ni PGDE ya open university tu ili niwe kuendelea na shughuli zangu binafsi
 
....... lakn nataman sana siku moja nipate ajira serikalini kwani kuna security.

Kuamua kufanya kazi serikali si kitu kibaya ila sababu ndiyo mbaya, ushauri wa kwanza ni wewe kuachana na hiyo kitu kwenye red.
 
Ukimaliza postgruate diploma ya ualimu unakuwa na SIFA sawa na za mwalimu wa digrii i. Hivyo serikalini utalipwa basic salary ya sh. 589000 kama mwl wa digrii. DUCE hiyo program ipo tena ni ya jioni. Huwa inachukua miezi 8 na ada ni sh. 3.5 millions. Nawasilisha.
 
Unaajiliwa kama kawa, ila kwa ushauri wangu komaa na kujiajili!

Hivi kwann lugha yetu kiswahili inatushinda kias hiki..?? Tatizo ni nini, elimu au ujinga..?? Speaking of Ajila, kujiajili, mpka kero yaan. Sio siri Baadhi ya Watanzania mnatuangusha sana for real.
 
Back
Top Bottom