Nimetajiwa shilingi milioni tano mahali ya kuoa

Nimetajiwa shilingi milioni tano mahali ya kuoa

joss1973

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2010
Posts
405
Reaction score
102
WaJF naomba ushauri wenu nifanye je ?

Mchumba nampenda sana na nataka kuoa ila hiyo mahari niliyotajiwa imeniumiza kichwa kabisa.

Wazazi wake wanataka mahari 5mil.mi ntatoa wapi ?

Hii ni biashara ?mbona tunaumizana hivi ?nimejaribu kuzungumza na mchumba wangu ,anasema hana uwezo wa kubadili maamuzi ya kikao cha wazazi na ndugu zake ? Naomba wajf mnishauri please?

Nifanye je?

Naomba ushauri
 
Huwez thaminisha personality ya mtu, life, education..... kwa pesa! Sijui valuer atatumia formula gani..
 
Ndoa ni utu (kujitoa) wala hakuthaminishwi na fedha kiufupi tu hawakutaki uoe but una chance moja tu....piga mimba lazima waje wapunguze dau

Ha hahahhaha! Ukifanya hivyo unavyoshauri, kwenye mahari aliyotajiwa ongeza na laki mbili nyingine.

Mahari ni makubaliano yanayowekwa so wahusika wa upande wako wazidi kujadiliana kulingana na uwezo wako
 
Kaka mahali ni muhimu... Familia ya mwanamke inakujaribu kupitia mahali. Kwamba kama huyu jamaa kweli ana uwezo wa kumtunza mwana wetu basi atoe kiasi fulani. Sasa hapo inaonesha ukichukua mtoto wa watu hata kupata hiyo milioni tano itakuwa shida kubwa sana. Hicho kiasi inawezekana ni kikubwa kwako. Ila kama kikubwa nenda kaangalie familia nyingine. Unataka kuchuma tunda tawi usilolifikia. Sehemu nyingine wanatoa watoto wao bure. Unaweza jaribu huko uone kwanini wanatoa watoto wao bure. Halafu ukioa familia nzima inahamia kwako. Utajua jinsi ya kuwapeleka shule na kuwyapa mitaji.
Usiseme nampenda nampenda tu, kwani hata tukishaoa na kuolewa tunapenda wangapi. Kuna maisha zaidi ya kupenda. Uzuri ukioa style ya huyo mwanamke unajifungia hata geti. Familia zao hazina tabia ya kutaka misaada kwa dada zao. Sasa mwenzangu kwa jinsi unavyolalama ukishaoa ukapata watoto utawapeleka wapi shule. Au ndio ile ya kusema tutajenga kwanza maisha. Kama bado hujajiandaa, usioe kwanza; jipange vizuri utaoa baadaye. Usikimbilie ndoa kama hujajipanga vizuri...
 
Nnachofahamu mahari sio lazima ilipwe yote na kuna nafasi kubwa tu kwa pande zote kujadili.
 
Lipa bride price kaka. You may now kiss the bride. She is your property lock,stock and barrel, to use and abuse.
 
Mahari ni kiashiria tu kwamba binti unayemchukua ana thamani fulani. Kwa desturi ya Afrika(sababu nimeiona hata south afrika),mahari huwa haimaliziwi kulipwa yote(si lazima umalize kulipa mpaka senti ya mwisho).Lengo kuu ni mme apate mke na mke apate mume,mtunziane heshima na mjenge familia. Makabila mengi ya tanzania kma sasa mahari wanafikisha mpaka 2m bila kuweka vile vifaa vingine!. Kama unampenda mke nae anakupenda,waambie washenga wa bargain kidogo ikishuka kidogo,kubali kisha lipa robo au nusu ya cash,iliyobaki waambie utapeleka siku zijazo. Wengi tumeoa kwa style hiyo na hakuna mgogoro. Mke ana heshima,thamani na utamu wake ndugu,ingawa halinganishwi na hatakiwi athaminishwe kwa thamani ya pesa
 
Kama anakupenda sana muibe mpotee mkajifiche sehemeu muanze maisha

Baada ya kama miaka 10 rudini na mtoto/watoto wenu mkawasalimie
 
WaJF naomba ushauri wenu .nifanye je ?? Mchumba nampenda sana na nataka kuoa ila hiyo mahali niliyotajiwa imeniumiza kichwa kabisa .wazazi wake wanataka mahali 5mil.mi ntatoa wapi ?? Hii ni biashara ??mbona tunaumizana hivi ??nimejaribu kuzungumza na mchumba wangu ,anasema hana uwezo wa kubadili maamuzi ya kikao cha wazazi na ndugu zake ?? Naomba wajf mnishauri plz??Nifanye je ??Naomba ushauri

Ni mahari sio mahali......ulijitambulishaje kwao je uliwaambia unamaduka kariakoo au uliwambia unafanya kazi ktk makumpuni makubwa na mshahara mnono au wanataka ushindwe wamuoze kwa mwenye nazo?pole sana hapa ndipo wazazi ukitangaza ndoa kwa binti zao wanataka kumaliza shida zao zote kwako dawa yao kumpachika mimba binti yao watakukususia
 
kaka yangu aliambiwa apeleke kilo kumi za dhahabu kwa kuwa yeye anatoka africa, akamwambia mchumba wake hata gram mia sitoi rudi nyumbani, demu akang'ang'ania kwa bro, mara mimba ya kwanza, mtoto hajatembea vizuri mimba ya pili, ooh wazazi wakasema jamani fungeni ndoa mahari mtalipa kidogo kidogo tuu na mfumo wa mahari ukabadilishwa. muda mwingine mahari kubwa unayolipiwa msichana inaenda kukupa maisha ya tabu huko. pole kaka wewe peleka hata milioni moja waambie wataendelea kukudai mwishoe mnajukuu
 
Ha hahahhaha! Ukifanya hivyo unavyoshauri, kwenye mahari aliyotajiwa ongeza na laki mbili nyingine.

Mahari ni makubaliano yanayowekwa so wahusika wa upande wako wazidi kujadiliana kulingana na uwezo wako

(Kwa Waislam) mahari ni haki ya mke mtarajiwa, yeye anaweza kuwaambia wanafamilia kuwa mahali yangu ni Tsh500/-, na hamna wa kuleta objection! Hili swala la mahari kutolewa mimacho mara kaka, mara mjomba ni upotofu mkubwa. Ama kuhusu wenzetu( Wakristo) sina hakika kwamba nani ni mwenye maamuz ya mwisho kutaja kiwango cha mahari. Kwa Waislam, kisheria anae taka kuolewa ana jibu la mwisho la kiwango cha fedha au mali kwa ajili ya Mahari, ijapokuwa anaweza kuwashirikisha wanafamilia pia.
 
Hiyo chumba yako hapendi wewe. Dawa tumbukiza kitu ndiiiiiii halafu uone. Watakupa bure
 
kaka yangu aliambiwa apeleke kilo kumi za dhahabu kwa kuwa yeye anatoka africa, akamwambia mchumba wake hata gram mia sitoi rudi nyumbani, demu akang'ang'ania kwa bro, mara mimba ya kwanza, mtoto hajatembea vizuri mimba ya pili, ooh wazazi wakasema jamani fungeni ndoa mahari mtalipa kidogo kidogo tuu na mfumo wa mahari ukabadilishwa. muda mwingine mahari kubwa unayolipiwa msichana inaenda kukupa maisha ya tabu huko. pole kaka wewe peleka hata milioni moja waambie wataendelea kukudai mwishoe mnajukuu

Ha ha ha ha, hiyo kali kaka!
 
Back
Top Bottom