Nimetajiwa shilingi milioni tano mahali ya kuoa

Nimetajiwa shilingi milioni tano mahali ya kuoa

Ha ha ha ha, hiyo kali kaka!

kweli kademu kalikuwa kaelitrea kamechanganyika na kamarekani cheusi hali ndiyo ilikuwa hivyo kwa kaka yangu wa kwanza. ila mimi siyo kaka ni dada
 
Heshima ya mahali naona imeshuka kutwa watu kulalamika kama hauko tayari usioe au tafuta wengine ambao mahali hawataki au wanataka ndogo.
 
zamani mahari ilikuwa ng'ombe 50-100, ungekuwa na ka milioni tano kako usinge oa
 
Kulaleki mie 2mil nikagoma nao wakakomaaa nasikilizia maana siku hizi kuoa ni mtaji mkubwa
 
mwambie mpenz utamwoa ukipata hiyo hela alafu pili unaju maana halisi ya ndoa??
 
Kaka mahali ni muhimu... Familia ya mwanamke inakujaribu kupitia mahali. Kwamba kama huyu jamaa kweli ana uwezo wa kumtunza mwana wetu basi atoe kiasi fulani. Sasa hapo inaonesha ukichukua mtoto wa watu hata kupata hiyo milioni tano itakuwa shida kubwa sana. Hicho kiasi inawezekana ni kikubwa kwako. Ila kama kikubwa nenda kaangalie familia nyingine. Unataka kuchuma tunda tawi usilolifikia. Sehemu nyingine wanatoa watoto wao bure. Unaweza jaribu huko uone kwanini wanatoa watoto wao bure. Halafu ukioa familia nzima inahamia kwako. Utajua jinsi ya kuwapeleka shule na kuwyapa mitaji.
Usiseme nampenda nampenda tu, kwani hata tukishaoa na kuolewa tunapenda wangapi. Kuna maisha zaidi ya kupenda. Uzuri ukioa style ya huyo mwanamke unajifungia hata geti. Familia zao hazina tabia ya kutaka misaada kwa dada zao. Sasa mwenzangu kwa jinsi unavyolalama ukishaoa ukapata watoto utawapeleka wapi shule. Au ndio ile ya kusema tutajenga kwanza maisha. Kama bado hujajiandaa, usioe kwanza; jipange vizuri utaoa baadaye. Usikimbilie ndoa kama hujajipanga vizuri...

hapo bado makorokocho ya harusi magharama ya nguo..sherehe..honeymoon....HUKO NI KUKOMOANA......umetetea ujinga.
 
WaJF naomba ushauri wenu .nifanye je ?? Mchumba nampenda sana na nataka kuoa ila hiyo mahali niliyotajiwa imeniumiza kichwa kabisa .wazazi wake wanataka mahali 5mil.mi ntatoa wapi ?? Hii ni biashara ??mbona tunaumizana hivi ??nimejaribu kuzungumza na mchumba wangu ,anasema hana uwezo wa kubadili maamuzi ya kikao cha wazazi na ndugu zake ?? Naomba wajf mnishauri plz??Nifanye je ??Naomba ushauri

mgonge mimba fasta uone kama mzigo hautopungua huo..atleast ulishaonesha nia
 
hiyo ni mahali ya mwanamke wa kawaida au malaika? Yaan utadhani unamnunua milele
 
WaJF naomba ushauri wenu .nifanye je ?? Mchumba nampenda sana na nataka kuoa ila hiyo mahali niliyotajiwa imeniumiza kichwa kabisa .wazazi wake wanataka mahali 5mil.mi ntatoa wapi ?? Hii ni biashara ??mbona tunaumizana hivi ??nimejaribu kuzungumza na mchumba wangu ,anasema hana uwezo wa kubadili maamuzi ya kikao cha wazazi na ndugu zake ?? Naomba wajf mnishauri plz??Nifanye je ??Naomba ushauri

Mkuu hilo dau ni kubwa sana ,ongea na gfriend wako washuke hata 2 m ,otherwise tafuta kwengine
 
(Kwa Waislam) mahari ni haki ya mke mtarajiwa, yeye anaweza kuwaambia wanafamilia kuwa mahali yangu ni Tsh500/-, na hamna wa kuleta objection! Hili swala la mahari kutolewa mimacho mara kaka, mara mjomba ni upotofu mkubwa. Ama kuhusu wenzetu( Wakristo) sina hakika kwamba nani ni mwenye maamuz ya mwisho kutaja kiwango cha mahari. Kwa Waislam, kisheria anae taka kuolewa ana jibu la mwisho la kiwango cha fedha au mali kwa ajili ya Mahari, ijapokuwa anaweza kuwashirikisha wanafamilia pia.

Nahisi hata wakristo ndivyo inavyotakiwa kuwa. Tatizo ni ufukara, kama utakuwa umegundua mara nyingi familia masikini huwa wanatoza mahari kubwa sana nafikiri huwa wanaona kama ndo pakutokea, lakini ni mara chache sana kuona familia ambazo zinajiweza zikakupiga mahari kubwa.

kaka yangu aliambiwa apeleke kilo kumi za dhahabu kwa kuwa yeye anatoka africa, akamwambia mchumba wake hata gram mia sitoi rudi nyumbani, demu akang'ang'ania kwa bro, mara mimba ya kwanza, mtoto hajatembea vizuri mimba ya pili, ooh wazazi wakasema jamani fungeni ndoa mahari mtalipa kidogo kidogo tuu na mfumo wa mahari ukabadilishwa. muda mwingine mahari kubwa unayolipiwa msichana inaenda kukupa maisha ya tabu huko. pole kaka wewe peleka hata milioni moja waambie wataendelea kukudai mwishoe mnajukuu

Hahahahaaaaa duh, Kg 10 za dhahabu kwa haraka haraka ni kama Mil 500 tsh kwa mahari tu!! Pambafu!!!
Mkuu kwani huyo shemeji yako ni mzungu ama??
 
just be man enough to face them and tell them you don't have that money and for now you can pay like 1mil then tell them you will finish later after weeding! After weeding no one would come and remind you about it, wakikataa mweke binti pending! But convice that lady to be on your side no matter what
 
kaka yangu aliambiwa apeleke kilo kumi za dhahabu kwa kuwa yeye anatoka africa, akamwambia mchumba wake hata gram mia sitoi rudi nyumbani, demu akang'ang'ania kwa bro, mara mimba ya kwanza, mtoto hajatembea vizuri mimba ya pili, ooh wazazi wakasema jamani fungeni ndoa mahari mtalipa kidogo kidogo tuu na mfumo wa mahari ukabadilishwa. muda mwingine mahari kubwa unayolipiwa msichana inaenda kukupa maisha ya tabu huko. pole kaka wewe peleka hata milioni moja waambie wataendelea kukudai mwishoe mnajukuu

Hebu twende taratibu kwanza usitukokotekotete tu, huyo kaka yako aliambiwa atowe mahari ya kilo 10 ya dhahabu kwa sababu anatoka Africa, je ni bara gani hilo alilokwenda kuoa na ni nchi ipi hiyo? ebu tuanzie hapo kwanza.
 
Wape makavu live. Waambie it's over una mambo mengi ya kufikiria. Hiyo mahali waliyokutajia itakuongezea mawazo yasiyo ya msingi.
 
WaJF naomba ushauri wenu nifanye je ?

Mchumba nampenda sana na nataka kuoa ila hiyo mahali niliyotajiwa imeniumiza kichwa kabisa.

Wazazi wake wanataka mahali 5mil.mi ntatoa wapi ?

Hii ni biashara ?mbona tunaumizana hivi ?nimejaribu kuzungumza na mchumba wangu ,anasema hana uwezo wa kubadili maamuzi ya kikao cha wazazi na ndugu zake ? Naomba wajf mnishauri please?

Nifanye je?

Naomba ushauri

Sasa hapo "mahali" ulitaka pawe million ngapi? Si unajuwa ardhi imepanda bei siku hizi.

Au ulimaanisha "mahari"?

Punguani wahed.
 
Back
Top Bottom