Nimetakiwa kuwa na kibali cha ujenzi

Nimetakiwa kuwa na kibali cha ujenzi

Drydon

Senior Member
Joined
Mar 11, 2019
Posts
125
Reaction score
191
Nimejichanga miaka kadhaa hatimae nikapata kakiwanja kangu huko ndanindani Zingiziwa

Nikajichanga tena wazo ni angalau niwe na kakibanda hata kamgongo wa ng'ombe nisahau adha za kodi. Juzi nimeenda na fundi wangu angalau tugawane rizk tumeanza kuchimba msingi leo tumeanza kuingiza tofauri kwenye msingi.

MAMA KAZUBI na wadau kadhaa[emoji1787] wananiwekea kauzibe wananidai kibali cha ujenzi dah chumba kimoja wallah. Nikagomea urahisishwaji sasa nimepewa barua ya wito kesho kwa mtendaji na msisitizo nisitishe ujenzi kwa sheria ya 1982[emoji58] je! Huwa kinajili nini na kuna gharama kiasi gani.
 
Nenda tu kuwa mpole kamsikilize mtendaji maana yeye ndio boss wa hilo eneo, omba utaratibu wa kupata kibali, jifanye mjinga maisha yaendelee, usilete ujuaji kwenye mitaa ya watu, usisahau kumpa hata 20 mtendaji.
 
Nenda tu kuwa mpole kamsikilize mtendaji maana yeye ndio boss wa hilo eneo,omba utaratibu wa kupata kibali, jifanye mjinga maisha yaendelee,usilete ujuaji kwenye mitaa ya watu, usisahau kumpa hata 20 mtendaji.
20 ya kiwaki sana half siyo unyama kabisa chamsingi anielekeze tu utaratibu niuzingatie ila haya masuala ya 20 hapana
Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
Sasa si unaenda tu kwa mtendaji na elfu 50 yako tatizo limeisha, sasa hivi hata ukijenga choo lazima uwe na kibali
 
Mitaa ya kipuuzi sana hiyo...mtendaji anataka apewe pesa...usipompa anawaleta manispaa, wale jamaa wa manispaa huwa wanawapa 15k..
Kama huwezi kupata kibali, mpe tu hyo 20k ujenge
 
Kama eneo lako halijapimwa (unsurveyed plot) kibali chake hakina usumbufu wala gharama sana, nenda tu ukawasikilize walichokuitia ikiwezekana uwapooze ili uendee na ujenzi wako
 
Hapo wanataka tu hela ya kula sikukuu hii mkuu usipotii wito ni adhabu nyingine na dau la hela linaongezeka
 
Halmashauri ya wapi maana kila halmshauri ina by laws zake
 
Mtafute mtendaji mpe hela ya chai uendelee kujenga otherwise endelea kulipa kodi ya nyumba. Na hapo bado siku ya kuweka maji na umeme utaratibu ni huo huo unalipia huduma unazungushwa unatoa hela unawekewa huduma siku hiyo hiyo
Nchi ya kitu kidogo
 
Usifinye sana mkono.. Hizi ni housekeeping rules za kuishi hii dunia.

Ukiwaza sana haya mambo utachukia kuishi maana yapo kila mahali
 
Kuna fundi yupo Zingiziwa yeye huwa anasema mambo ya kibali nitadeal nayo mwenyewe...utakuwa hujabahatika kukutana na huyo

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nimejichanga miaka kadhaa hatimae nikapata kakiwanja kangu huko ndanindani Zingiziwa

Nikajichanga tena wazo ni angalau niwe na kakibanda hata kamgongo wa ng'ombe nisahau adha za kodi. Juzi nimeenda na fundi wangu angalau tugawane rizk tumeanza kuchimba msingi leo tumeanza kuingiza tofauri kwenye msingi.

MAMA KAZUBI na wadau kadhaa[emoji1787] wananiwekea kauzibe wananidai kibali cha ujenzi dah chumba kimoja wallah. Nikagomea urahisishwaji sasa nimepewa barua ya wito kesho kwa mtendaji na msisitizo nisitishe ujenzi kwa sheria ya 1982[emoji58] je! Huwa kinajili nini na kuna gharama kiasi gani.
Mkuu @drydone umepata hati ya kiwanja?

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
20 ya kiwaki sana half siyo unyama kabisa chamsingi anielekeze tu utaratibu niuzingatie ila haya masuala ya 20 hapana
Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
Ni rahisi sana kufuata utaratibu, nenda Halmashauri pamoja na ramani ya nyumba yako, ingia Idara ya Mipango Miji watakupa utaratibu. Kibali cha ujenzi ni bei rahisi sana, nadhani haizidi elfu 50 kwa nyumba ya kawaida. Kama michoro yako imekaa vizuri, ni ndani ya siku saba za kazi kibali kinakuwa kimetoka. Mheshimu Mtendaji Kata na umpe ushirikiano, tambua kuwa hafanyi kwa matakwa yake bali kwa mujibu wa sheria za nchi na sheria ndogo za Halmashauri; na waliotunga hizo sheria na taratibu ni wawakilishi ambao tuliwachagua sisi wenyewe. Kazi yake ni kusimamia tu hizo taratibu, wala hajatunga yeye. Aidha, zingatia kuwa Mtendaji Kata ndio anatekeleza majukumu ya Mkurugenzi wa Halmashauri kwenye kata hiyo, hivyo usiwe miongoni mwa wanaorudisha nyuma maendeleo ya Halmashauri yako.
 
Naomba Kujua Kibali Cha Ujenzi Ni RURAL areas au Ni URBAN Areas?

Kama Ni Urban Areas tuu inakuwaje Huku REA tunadaiwa kibali cha ujenzi?
 
Back
Top Bottom