Nimetembea mikoa mingi Tanzania nimegundua kuwa Dodoma kuna nyoka wengi hatari kuliko mikoa yote Tanzania

TABORA imezidi jamani hasahasa wilaya ya Urambo Kuna nyoka hatari huwezi kutembea bila kukutana na nyoka zaidi ya mmoja
 
Wafuge nyani na tumbili nguchiro na jamii zake ili kuwapunguza hao nyoka.
Ila madhara nyoka wakipungua mavuno yatapungua mashambani kwa sababu ya panya watakuwa wengi sana.
Nyoka maporini wanasaidia kufanya ecologia ya panya wasiwe wengi wakaathiri mavuno mashambani.
 
Hizo aina zote unazozisema zinapatikana Tabora, karibu kwetu Tabora napo ujifunze ndio utajua huku ndio genesis ya hao wadudu
 
Sikupingi hata kidogo.Mimi niliwahi kwenda Mpwapwa kwa ajili ya field practices za mambo ya upimaji ardhi.Tulikuwa tunafanyia maporini huko kwenye mibuyu kibao.Aisee nilikumbana na nyoka wa kila aina ya rangi.
Hii ni komenti nilitaka nione, kaka Mpwapwa kuna Nyoka wengi. Mi nimesoma huko chuo duuh hatar... Hao wote Aliowataja nilikutana nao.

Siku moja watu wanajisomea, nyoka mrefu aina ya cobra alikuwa analeta shida kitaka kuingia library tukafunga milango,cwengine walikuwa nje wakimpiga, alikuwa na hasira mno na kufoka kwa sauti kubwa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…