Ni kwamba nilikuwa ugenini, nikakutana na mdada ambaye niliona kama niliwahi kuonana naye Tz, wakati tunaongea akanambia ametokea jijini Dar, nami nikamwambia nilikotokea kuwa ni Mz, wakati wa maongezi marefu ndo kanambia kuwa anahitaji kupata sehemu ya kupumzika, nikamkaribisha hotelini nilikofikia. Mambo yakaendelea kama kawaida nikimwita mpenzi. Siku ya siku Bro akakumbana na namba yangu kwenye siku yake, akamhoji alipataje namba yangu - binti akajikanyaga. Bro aliponipigia mimi na kunihoji kuhusu binti huyo nikamwambia ukweli kuwa ni mchumba wangu. Sasa Bro tayari ana mtoto mmoja na huyo binti na anamtishia kumuacha, binti analalamika kuwa nimemwalibia maisha. Haya nipeni ushauri.