Nimetengwa baada ya baba yangu kufariki


splendid advice!
 
Lukas...sijasema ujitenge namaanisha uendelee na maisha yako bila kujari kuna mtu mwingine au la...ni bahati mbaya watu hatuweki baadhi ya mikasa yetu...ninauona wako mdogo sana ukilinganisha na wa kwangu...lkn nasonga!!

pamoja na hayo mkuu, jamaa anayo haki ya kisheria, kikanuni na kikatiba ya kupata urithi kutokana na mali za baba yake. kwanini wengine wapate, yeye akose? haikubaliki hata kidogo. lazima naye apate walau ekari 1 kutoka mashamba ya babaye na mgawo wa mali zingine...ni haki yake ya MSINGI.
 
Last edited by a moderator:
You have a point. Watoto wote wana haki ya kupata huduma kutoka kwa wazazi wao. Kwa vyoyote vile, unahitaji msaada wa mzazi ili upate msingi wa kujitegemea. Kama ulikuwa unakaa naye, na hapakuwa na wosia aliandika, na ndugu zake walikuwa wakikuona, na walitambulishwa ila sasa wamegeuka kwamba hawakutambui, ni ubinafsi tu na uchoyo wa mirathi.

Nenda ofisi za ustawi wa jamii, watakushauri nini ufanye. Lakini pia, usisahau kuomba kipimo cha DNA, ili kuondoa argument yao kwamba wanakuondoa kwenye orodha ya ndugu kwa vile hawakufahamu. kuanzia hapo, DNA ikishatoka, utakuwa na mwanzo mzuri wa ku claim sehemu yako kama mwanafa milia.

Ninaomba wana forum wengine tumsaidie ushauri kijana ili apate haki zake za kuzaliwa zimsaidie angalau kumaliza elimu yake ya awali ili aweze kujitegemea.


 

tpaul usemayo ni kweli...lkn kama ndugu washamsusa itachukua muda na resource kupata haki yake...kama anaweza kuishi kwa nini atumie nguvu kutambuliwa kama mwanafamilia...kwa nini asitafute tu ya kwake...
 
Last edited by a moderator:
utachukua muda na pesa nyingi kugombea urithi, utajihatarisha bure. wewe uko chuo mbona umeshasimama! Tafuta maisha, amini nakwambia hao ndugu wanaotegemea pango la nyumba zilizojengwa miaka hiyo watakuja kwako kutaka msaada. PIGA KAZI.
 
Hizo sio zako ndugu.Wewe jenga tu undugu kama watakusaidia sawa wasipokusaidia sawa.Utatafuta namna zingine.

Na huna haki ya kuwalaumu hao, mlaumu Babako kwa kutokukuandalia kabla.
 
agombee undugu kwa watu wasiomtaka ili iweje? mali ndio muhimu...naye ni mtoto halali wa marehemu na anastahili kupata urithi kama watoto wengine. acha kumtia mwenzako unyonge.

Hana haki ya kudai lolote hapo, anahitaji kudra tu wamsaidie ila HAKI HANA.

Hivyo suala la kwenda nae kisheria hapati kitu.Huu ndio ukweli japo mchungu.

So muhimu kwake kama anahitaji undugu ajenge undugu vinginevyo hana lake hapo.
 
Najua huruma uliyoipata lakin umeenda mbali sana.

Hao wamepata mali ya dhuruma kivip?huyo Baba alikuwa anaishi na hiyo familia yake na mke wangu, mali ya ndoa ni ya mke na mme, sasa mme kaondoka hivyo sasa mali ni za mke au watoto wa ndoa. Na huyu wao hawamtambui, sasa wameiba vip?unamewaonea bure.
Suala hapa ni Baba ndio alichemsha, alipaswa ajue haya tatatokea hivyo kama ni kumpa angempa akiwa hai, kwa kuwa Baba yake hakumoa unataka hawa wengine wampe mtu wa nje kwa sababu gani?kwa wema gani walionao ambao Baba yake hakuwa nao?Ni sawa nawe uwe na mme, mkachuma mali kadhaa na mkazaa watoto ndani ya ndoa, zile mali mlizopata ndani ya ndoa sio za baba tu kama anavyofikiri huyu, ni mali za ndoa yaan za mme na mke wa ndoa, hivyo mtoto wa nje ya ndoa uwa hawi considered.Huyo ni wa Baba binafsi hivyo Baba kwa mali zake binafsi zisizo za ndoa angempa huyo mtoto akiwa hai au angeandika will kwa mali zake binafsi ambazo kwa maelezo yake hapo hakuna kitu kama hicho, hivyo hana namna ya kudai mali kwa sasa. Kama hao watoto wa ndoa wakitaka asipate chochote hatapata na ni haki yao, ni mali ya pamoja ya Baba na Mama yao, haajamuibia wala kumdhurumu hapo.


Ndio maana hapa aamue tu kujenga undugu, by the way kasema ana mchumba anayetaka kumuoa, hii maana yake ni mtu mzima, hakuna njia moja ya mafanikio, afungue macho njia zingine zitaonekana.
 
Okey, but father na motherless died at the same time there is no mother mkubwa.
Thanks.

Then hapo watoto wa ndoa watakuwa na haki kuliko wewe, maana mali yoyote ni ya Baba yao na Mama yao
so kama Baba yako hakufanya lolote kabla huna haki ya kupambana nao kisheria, na hutawashinda.

Jenga undugu, kama watakusaidia kwa wema shukuru wasipokusaidia Mungu ni mwema utapata namna nyingine.
 
HAKI HAMNA HAPO NDUGU, zaidi atajipotezea muda tu.

Kumbuka kuacha mwenyewe utajijengea heshima zaidi kuliko kupigana vita ambayo huwezi shinda.
 
Kikubwa zaidi, ichukulie umri umefika wa kuoa, mke mtarajiwa anasema nami natamani kuja kwenu kwa wazazi wako, kwa mtazamo wako unafikiri nitampeleka wapi akidai twende kwa baba mzawa! Just help,

Kama ulivyosema.

Tayari una mke mtarajiwa, hivyo unaweza kujisimamia.

Songa mbele utafanikiwa.Fahamu hili mali yoyote ni ya mme na mke, wewe huhusiki na mke wa huyo jamaa, wewe sio mtoto wa ndoa, na mali zile ni zao ndoa, hivyo watoto wa ndoa huwezi kuwashinda.

Watakushinda tu kisheria.
 
Mkuu Bosco Saronga Makoi kwa jinsi nilivyomsoma na kumwelewa lucas4 sidhani kama unamshauri vizuri.Ni hivi watoto wa nje ya ndoa sheria inawanyima haki sasa unapomwambia akomae sijui unataka akomae vipi wakati akienda mahakamani ataulizwa minutes za kikao cha ukoo ?.Ka vyovyote atakuwa hana na kama mashangazi na wababa wadogo na wakubwa wameshamgomea ndio basi ni bora akajitafutia riziki na kusahau mambo ya Baba.


Pambana mkuu uhakikishe haki yako imepatikana. Hao wanao kuambia achana uachane na familia yako ambayo kimsingi ni muhimu kuijua
Hata kama haitakusaidia kitu.

KomAa nao kisheria.
 
Last edited by a moderator:
kufahamiana kwao na mama ni kwamba kulikuwa kuna kaka wa kwanza alikufa mbaye alikuwa mkubwa kwangu ndiyo huyo wao ndio wanadai kuwa angekuwa yule wa kwanza wangekubaliana nae ila sio mimi,tatizo ndio hlo.

Basi wanajua wewe sio damu yao ila huyo kaka yako alikuwa ni damu yao. Watakuwa wanajua uhusiano wa mama yako na mwanaume mweingine ndio wewe ukazaliwa. Ungekuwa umekataliwa na huyo mama wa kambo tungesema ana roho mbaya lakini kama ni shangazi na baba mdogo fuatilia vizuri umjue baba yako wa ukweli. Kupiga picha au kusomeshwa na baba yakp sip kigezo kama wewe ni wake labda alifanya hivyo kwa upendo wake tu.
 
Kikubwa zaidi, ichukulie umri umefika wa kuoa, mke mtarajiwa anasema nami natamani kuja kwenu kwa wazazi wako, kwa mtazamo wako unafikiri nitampeleka wapi akidai twende kwa baba mzawa! Just help,

Si umwambie ukweli wa status yako from the beggining? Sidhani kama atadai umpeleke kwa wazazi wako wakati uliisha mwambia hali halisi.
 
The moral of this saga is be a father to your child, and if you don't want children or can't provide for them, wrap it up or something.
 

Kama umeuelewa vizuri uzi huu ni kwamba, mkataliwa alishawahi kuishi nao nyumba moja wakati baba yake akiwa hai na walitambulishwa na kuelewa hilo. Alifukuzwa/kukataliwa baada ya baba kufa. Unapaonaje hapo sio kudhurumiwa/kuibiwa haki??
 
Kama umeuelewa vizuri uzi huu ni kwamba, mkataliwa alishawahi kuishi nao nyumba moja wakati baba yake akiwa hai na walitambulishwa na kuelewa hilo. Alifukuzwa/kukataliwa baada ya baba kufa. Unapaonaje hapo sio kudhurumiwa/kuibiwa haki??
Msome vizuri, amesema amekaa hapo kwa wiki 2 tu kabla Baba hajafa, Mama yake hakuwa mke, huyo Baba alikuwa na mke wake sa ndoa, mali alichuma kwenye ndoa yake ndoa ambayo ina watoto pia.

Hivyo hizo mali hazikuwa za Baba tu, bali ni za Baba na Mke wake ambaye sio mama wa huyo.

Sasa atachukuaje urithi wa Mama wa wenzake?kudai tu na kuanza kupeleleza kuna mali kiasi gani ni dalili za uroho wa mali na kuwa shida yake ni mali na sio undugu kama kichwa cha habari kinavyosema.

Mie pia ni Baba mwenye mtoto nje ya ndoa, na niliomba ushauri wa kisheria na hiki ndicho nilichoambiwa na mwanasheria, kuea mtoto wangu wa nje hana haki ya mali yoyote ya ndoa yangu, bali atakuwa na haki labda ya mali yangu binafsi isiyo ya ndoa, ndivyo sheria zilivyo kwani mali ya ndoa sio mali ya Baba binafsi na sio mali ya watoto bali ni mali ya ndoa(Baba na Mama); so kama wana ndoa hao hawapo moja kwa moja watoto wao watakuwa na haki na mali za wazazi wao unless wazazi hao kwa pamoja waseme otherwise.

Ndio maana huyo Baba bila shaka alikuwa anajua hilo pia, kama angekuwa ana nia ya kumpa shamba au nyumba ni wazi kuwa angemfanyia hivyo akiwa hai, lakin kama ata Baba wadogo,Baba wakubwa na mashangazi wanamkatalia then jua wanajua kuwa Baba yake mwenyewe hakuwa na mpango wa kumpa hizo mali anazozililia.
 
Hapa ndipo umuhimu wa mke mmoja, mtoto mmoja unapokuja.

Hakuna chance ya watoto kugombea mali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…