Najua huruma uliyoipata lakin umeenda mbali sana.
Hao wamepata mali ya dhuruma kivip?huyo Baba alikuwa anaishi na hiyo familia yake na mke wangu, mali ya ndoa ni ya mke na mme, sasa mme kaondoka hivyo sasa mali ni za mke au watoto wa ndoa. Na huyu wao hawamtambui, sasa wameiba vip?unamewaonea bure.
Suala hapa ni Baba ndio alichemsha, alipaswa ajue haya tatatokea hivyo kama ni kumpa angempa akiwa hai, kwa kuwa Baba yake hakumoa unataka hawa wengine wampe mtu wa nje kwa sababu gani?kwa wema gani walionao ambao Baba yake hakuwa nao?Ni sawa nawe uwe na mme, mkachuma mali kadhaa na mkazaa watoto ndani ya ndoa, zile mali mlizopata ndani ya ndoa sio za baba tu kama anavyofikiri huyu, ni mali za ndoa yaan za mme na mke wa ndoa, hivyo mtoto wa nje ya ndoa uwa hawi considered.Huyo ni wa Baba binafsi hivyo Baba kwa mali zake binafsi zisizo za ndoa angempa huyo mtoto akiwa hai au angeandika will kwa mali zake binafsi ambazo kwa maelezo yake hapo hakuna kitu kama hicho, hivyo hana namna ya kudai mali kwa sasa. Kama hao watoto wa ndoa wakitaka asipate chochote hatapata na ni haki yao, ni mali ya pamoja ya Baba na Mama yao, haajamuibia wala kumdhurumu hapo.
Ndio maana hapa aamue tu kujenga undugu, by the way kasema ana mchumba anayetaka kumuoa, hii maana yake ni mtu mzima, hakuna njia moja ya mafanikio, afungue macho njia zingine zitaonekana.