Dx and Rx
JF-Expert Member
- Jul 16, 2017
- 1,323
- 3,143
Heri ya Sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya wana JamiiForums wote. Bika shaka mpo salama na mnaendelea vyema na heka heka za kusherehekea hizi sikukuu, kwa wale wenye changamoto za hapa na pale, Mungu awatangulie.
Kama kichwa cha uzi kinavyosomeka, mwaka huu umekuwa ni mwaka mwema(mzuri) sana katika historia ya maisha yangu kwani umekuwa ni mwaka wenye milango ya riziki kufunguka na kuwa na uhakika wa milo 2 kwa siku.
Nimejitathmini kwa kipindi cha kuanzia February hadi mwezi huu kwa kuchakata data za matumizi yote ya kila siku ikiwemo Malazi(kodi ya pango), Mavazi, Chakula na mengineyo(kusaidia ndugu, wazazi, michango ya harusi, rambirambi, ada za shule, n.k) nimepata matokeo kuwa ninatumia wastani wa 2.5M kwa mwezi. Najikaza kupunguza matumizi lakini wapi, ngoma inagoma.
Tushirikishane mbinu za kubana matumizi maana mbinu zangu zimegoma.