Nimetimiza miezi minne sasa bila kunywa pombe!

Nguvu moja

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2017
Posts
3,371
Reaction score
2,713
Ilikuwa nikipata pesa tu nikimaliza kutoa mahitaji madogo madogo nyumbani ikiwemo pesa za matumizi kwa mke wangu

Basi hata kama nitakuwa na laki mbili zote nitazimaliza bar kwa kujenga heshima... Kunywa na kuwanunulia jamaa na marafiki asubuhi yake sina hata sentano

Yalikuwa maisha mabaya sana kwangu mpaka roho nafsi yangu ilikuwa aiko sawa kwa uteketezaji huo wa pesa niliokuwa naufanya, lakini mwisho wa siku nikawa namuomba mwenyezi mungu aniepushie hilo janga

Hadi leo ninapoandika hii thread nina miezi minne na wiki mbili nimeacha unywaji wa pombe najiona niko mwepesi mapigo ya moyo yalikuwa kasi sana sasa moyo wangu umepoa kabisa nimeamua kuishi maisha mapya kabisa hata familia yangu nyumbani wamefurahi na kushukuru.

Shukran pekee nampelekea mwenyezi mungu kwa kunitoa juani na gizani na kunipeleka kivulini.

Nawasilisha.
 
Hapo watakao msingizia JPM eti ndie kakusababishia watachuma dhambi!!!
JPM hajatimiza miaka 4 tangu aingie madarakani.
Uliacha enzi "watu tunachezea" hela
 
unaacha vipi kunywa pombe ??
kampuni za pombe zitajiendesha vipi ??
rudi nyumbani kunakaribua kunoga bia buku inakuja

sio ndoto
Nashukuru mkuu nimefika kikomo kwa sasa

Kila jambo na wakati wake mkuu wasalimie mkoa wa mbagala bila kusahau
Kisuma bar mbagala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…